Makamu Wa Rais Afanya Mazungumzo Na Waziri Wa Biashara Wa Ufaransa |Shamteeblog.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya  mazungumzo na waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi  Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.

Katika mazungumzo yao, pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri ambao umedumu kwa muda mrefu hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuendelea kuimarisha uhusiano wa biashara kati ya pande mbili. Kupitia Waziri huyo Serikali ya Ufaransa imeahidi kuongeza kiwango cha fedha kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo katika sekta ya miundombinu, kilimo, afya na maji.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu wizara ya Afya – Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk N Mbarouk.


By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post