Mjane auawa kikatili kwa mgogoro wa kuishi eneo la familia ya marehemu |Shamteeblog.



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Watu wanne (wanafamilia) wakazi wa Lunguya kata ya Mtwango wilaya ya Njombe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauji kwa kumkata na vitu vyenye ncha kali Bi Emma Mfikwa (43) kutokana na kula njama za kufanikisha kuuawa kwa mjane huyo aliyekuwa na mgogoro na wanafamilia kwa kuishi nyumba aliyojenga na mume wake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema “Huyu mama,mume wake alijenga nyumba yake katika viwanja vya familia na watu wa familia ile hawakupenda huyu mama awepo eneo lile kukawa kuna mgogoro”alisema Kamanda Issa

Vile vile amesema mjane huyo ameuawa wakati akiendelea na kesi yake mahakamani dhidi ya migogoro hiyo.

“Na kesi zipo mahakamni zinazohusiana na umiliki wa hiyo nyumba,kabla kesi haijafika mwishoni mama ameuawa.Na kitu cha ajabu zaidi katika watu ambao wanatiliwa mashaka mtoto wake wa kumzaa mwenyewe ni mmojawapo.hawa wane tutawafikisha mahakamani ili haki itendeke kutokana na ukatili uliofanyika”alisema Kamanda Issa

Katika hatua nyingine kamanda Issa amesema jeshi hilo linasikitikana vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani humo kutokana na kuokota mwili wa mtoto wa takribani miezi 8 akiwa ametupwa kwenye bonde lisilo kuwa na maji.

“Mtoto huyu ameokotwa kwenye bonde la mto ambao hauna maji karibu na chuo cha meendeleo ya jamii,mtoto huyu ingawa amefunikwa vizuri lakini kwa ajili ya ubaridi ameokotwa akiwa amefariki”alisema Kamnda Issa

Aidha Kamanda wa Polisi amewataka wananchi kuacha vitendo hivyo vya ukatili kwasababu ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na kuileza jamii kuwa vitendo hivyo havikubaliki.


 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post