MUME ASAKWA NA POLISI TUHUMA ZA KUUA MKE BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA |Shamteeblog.


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Fausta Silayo (22), mkazi wa kijiji cha Samanga wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro ameuawa kwa kuchomwa kisu na mume wake kwa madai ya kumnyima unyumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa
mwanamke huyo ambaye bado alikuwa uzazi wa mwezi mmoja alichomwa kisu Julai 23,2021 na kufariki dunia Julai 24,2021 wakati akipatiwa matibabu Hospitalini.

"Chanzo cha tukio hili inadaiwa kuwa ni mtuhumiwa kunyimwa kushiriki unyumba Jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye inasemekana amekimbilia nchi jirani ili kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria",amesema Kamanda Maigwa.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post