Ayisha Togina ni mtumiaji wa Mtandao wa Facebook ambaye anasimulia kisa cha familia maskini ambayo baba mzazi wa mapacha wake wa kike anahangaika na maisha magumu akiwalea wanawe hao baada ya mwamba mmoja kuwapa mimba kwa mpigo kisha kuingia mitini.
Kwa mujibu wa Ayisha familia hiyo ya nchini Cameroon inaishi kwenye umaskini wa kutupwa na inahitaji msaada baada ya kubebeshwa mzigo huo wa kuwalea mapacha wake waliopewa mimba na jamaa mmoja.
Ayisha anasema baba yao mzazi hana kazi hivyo mabinti hao ili wapate kujikimu, waliingia mikononi mwa jamaa husika ambaye alifanya nao ngono wote wakapata mimba na akatoweka eneo hilo ambalo pia kulitokea migogoro ya kutumia silaha
Ayisha anasema kuwa, alipowaona mapacha hao na kuwauliza kulikoni, walimweleza yote na kuona wanaishi maisha magumu sana, akawaomba wamruhusu awapige picha na video ili awaombe watu na taasisi ziwasaidie kwani licha ya mimba walizonazo, bado wanafuatwa na wanaume walale nao kingono ili wapate pesa kidogo maisha yaende.
from Author
Post a Comment