Ujenzi wa daraja la kudumu la Kitengule lenye urefu wa meta 140 ukiendelea. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutaziunganisha wilaya za Karagwe na Misenyi Mkoani Kagera
Ukarabati wa miundombinu ya mizani ya Nyakahura iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Kagera, ukiendelea kwa kasi. Mizani hiyo inatumika kupima magari makubwa ya mizigo zaidi ya 400 kwa siku, yanayofanya safari zake kati ya Tanzania, Burundi na Rwanda
Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba Ruhoro (mwenye suti ya bluu), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (kushoto), wakati akikagua barabara ya Omubuga, Rulenge hadi Murugarama (KM 32), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto kwa mbunge huyo ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara Col. Mathias Kahabi.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiongea na wakazi wa kata ya Rulenge Wilayani Ngara, aliposimama kuzungumza nao wakati akikagua barabara ya Omubuga, Rulenge hadi Murugarama (KM 32), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati akikagua ujenzi wa daraja la Kitengule lenye urefu wa meta 140, na barabara unganishi (KM18), kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Col. Sakulo akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.PICHA NA WUU
Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Kagera Mhandisi Ntuli Mwaikokesa, akimkumbusha jambo Mhandisi Mkazi Charles Romisha, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa daraja la Kitengule na barabara unganishi (KM18). Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe.
By Mpekuzi
Post a Comment