Meneja wa msanii Young Lunya Petitman Wakuache amem-surprise mama wa mtoto wake Official Dodo baada ya kumvalisha pete ya uchumba katika chumba cha kujifungulia wajawazito leba.
Petitman Wakuache amepost video akimvalisha pete mpenzi wake akiwa leba huku akisindikiza caption inayosema ‘I love you Official Dodo mama yake Petit Junior’.
Petitman amefanya hivyo baada ya mpenzi wake huyo kujifungua mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la Petit Junior siku ya jana baada ya kushea habari hizo kwenye page yake ya instagram.
Huyo anakuwa mtoto wa pili kwa Petitman baada ya Baby Taraj wakuache aliyempata akiwa na Esma Platnumz.
from Author
Post a Comment