SAVANNAH PLAINS SCHOOL YATUA KWA KISHINDO KWENYE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA..YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO |Shamteeblog.

Meneja Masoko wa Savannah Plains School, Kennedy Karoli (kulia) na Afisa Masoko wa shule hiyo, Wema Kanyika wakionesha vifaa vinavyotumika kufundishia masomo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shule ya Sekondari Savannah Plains maarufu Savannah Plains School iliyopo Ibadakuli Mjini Shinyanga imeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha shughuli wanazofanya ikiwa ni pamoja na vifaa vya kisasa wanavyotumia katika kufundishia masomo mbalimbali.


Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye Maonesho hayo leo Julai 26,2021 Meneja Masoko wa Savannah Plains School, Kennedy Karoli amesema maonesho hayo ya yamewapa fursa ya kuonesha masomo na vifaa wanavyotumia kufundishia ‘Teaching aids’ vikiwemo vinanda (Piano), kwa ajili ya somo la Muziki, vifaa vinavyotumika kwa shughuli za sanaa na utamaduni, Swimming Program na kutoa elimu mbalimbali ikiwemo kuhusu Mbuga ndogo ya wanyama iliyopo shuleni.

“Pia tunatumia maonesho haya kutangaza Nafasi za masomo kwa wale wanaotaka kujiunga au kuhamia Savannah Plains School kwa mwaka wa masomo 2021 nafasi zipo kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Sita. Tahasusi zinazotolewa kwa upande wa Kidato cha Tano na Sita ni pamoja na HKL, HGK, HGL, HE, ECA, PCB,PCM,PGM na CBG”,amesema Karoli.

Amefafanua kuwa shule ya Savannah Plains School ina walimu waliobobea na kwamba wana ufaulu wa uhakika katika mitihani akitolea mfano kuwa katika matokeo ya Mtihani wa Utamirifu (Mock) Kidato cha Nne mwaka 2021 wameshika nafasi ya kwanza mkoa wa Shinyanga ikiwa mwaka huu ndiyo wanakuwa na darasa la kwanza kidato cha nne tangu shule hiyo ianzishwe.

“Kwa upande wa matokeo ya kidato cha Kidato cha Pili mwaka 2020 wanafunzi wote walipata daraja la kwanza. Hii inaonesha namna gani shule hii imejipanga vyema. Karibuni sana Savannah Plains School, Shule ni ya bweni ,tunapokea wanafunzi wa madhehebu yote na dini zote”,ameongeza Karoli.
Meneja Masoko wa Savannah Plains School, Kennedy Karoli akionesha shughuli mbalimbali zinazotolewa katika shule hiyo iliyopo Mjini Shinyanga kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja Masoko wa Savannah Plains School, Kennedy Karoli (kulia) akionesha Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2020 ambapo wanafunzi wote walipata Division One na katika matokeo ya Mtihani wa Utamirifu (Mock) Kidato cha Nne mwaka 2021 wameshika nafasi ya kwanza mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni  Mwalimu wa Shule ya Savannah Plains , Wema Kanyika ambaye pia ni Afisa Masoko wa shule hiyo.
Mwalimu wa Shule ya Savannah Plains , Wema Kanyika ambaye pia ni Afisa Masoko wa shule hiyo akionesha vifaa vya kisasa wanavyotumia kwenye shughuli za sanaa na utamaduni katika shule ya Sekondari Savannah Plains.
MMwalimu wa Shule ya Savannah Plains , Wema Kanyika ambaye pia ni Afisa Masoko wa shule hiyo akionesha vifaa vya kisasa wanavyotumia kwenye shughuli za sanaa na utamaduni na mambo mengine yanayofanyika katika shule ya Sekondari Savannah Plains.
Meneja Masoko wa Savannah Plains School, Kennedy Karoli akibonyeza Kinanda kinachotumika kufundishia muziki wanafunzi katika shule hiyo.Aliyesimama ni Mwalimu wa Shule ya Savannah Plains , Wema Kanyika ambaye pia ni Afisa Masoko wa shule hiyo.
Sehemu ya vifaa vinatumika kufundishia katika shule ya Sekondari Savannah Plains.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post