Shabiki Atoa Laki Mbili Atafutiwe Mzee Mpili |Shamteeblog.




KAMA masihara vile lakini huo ndio ukweli, baada ya shabiki mmoja mkazi wa Kigoma aliyejitambulisha kwa jina la Ma Beatrice shabiki wa Simba Kutamka wazi kuwa yupo tayari kuolewa na Mzee Mpili.

 

Shabiki huyo alikuwa anazunguka kila kona akisema kuwa anamtafuta Mzee Mpili ili aweze kuona uwezo wake ambao mara zote amekuwa akijitapa nao, huku akifunguka kuwa kama kweli mzee huyo ni mwamba aje awe naye.

 

Kwa kuonyesha kuwa yupo serious na jambo hilo, mama huyo alizungumza na Championi Jumatatu na kumtaka mwandishi amsaidie kumtafuta mzee huyo na akifanikiwa atatoa zawadi ya shilingi laki mbili.

 

“Kaka mimi namtaka Mzee Mpili, yeye si anasema ni mwamba mimi nipo tayari kuwa mke wake ili nione huo umwamba. Nitakupa laki mbili ukiniletea Mzee Mpili hapa,” alisema mama huyo.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post