Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kinaendelea kukabiliana na mapambano dhidi ya COVID-19 kwa vitendo na katika kuunga mkono juhudi za Marais wote wa Tanzania bara na Visiwani Zanzibar.
Akizungumza kwenye Maonesho ya Vyuo Vikuu ambayo yanasimamiwa na TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Mkuu wa kitengo cha Udahili katika chuo cha SUZA Ali Shauri Jecha amesema wao kama SUZA wanafuata maelekezo yote yaliyotolewa na Serikali na wataalam wengine wa afya.
Amesema kwenye Campus zao zote wameweka sehemu tofauti tofauti ambazo zinawafanya wanafunzi kunawa mikono yao kwa maji tiririka na sabuni na kwamba ni lazima kwa watu wote kuvaa barakoa.
Ali amengeza kuwa hata kwenye maonesho ambayo wao ni sehemu ya washiriki wana barakoa ambazo zimetengenezwa chuoni hapo na kuongeza kuwa wana vitakasa mikono (Sanitizer) ambavyo wana imani vitawasaidia vipindi vyote watakavyokuwa kwenye maonesho hayo.
Naye Khadija Sadiq Mahumba ambaye ni mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko amewakaribisha watu wote kutembelea wenye banda la SUZA kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo mbalimbali.
By Mpekuzi
Post a Comment