Ukuaji wa Sekta ya Bima yahitaji wataalam wenye Weledi |Shamteeblog.

*Chuo cha Uhasibu Arusha chapongezwa kuanzisha shahada Bima kwa Mfumo tofauti

Na Chalila Kibuda ,Michuzi
IMEELEZWA kuwa Sekta ya Bima kuweza kukua kiuchumi na biashara inahitaji watu wenye weledi na sifa wa kufanya kazi hiyo kwa utaalam.

Licha ya kukua kwa Sekta ya Bima, Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) imekuja na shahada ya Bima kwa mfumo wa Uanangezi wa kusoma na kufanya kazi sehemu zinazohusu sekta hiyo ili kwenda pamoja katika umahiri pindi anapohitimu.

Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Neema Lutula, wakati wa uzinduzi wa mtaala wa Bima na wanagenzi wa Chuo hicho ambao umeshirikiana na Shirika la Bima Tanzania(NIC)amesema wataalamu hawa watasaidia jamii kunufaika na uwepo wa sekta ya Bima katika uchumi na maisha yao ya kila siku ,hususani katika kupata elimu ya kinga na majanga mbalimbali kiuchumi na kijamii.

Alisema sekta ya bima inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo muamko mdogo wa wananchi kununua bima,huduma kuwafikia wananchi hususani wa vijijini na elimu ndogo masuala ya Bima kuhusu bidhaa tofauti za Bima.

"Kuanzishwa kwa mtaala huu utakuwa ni sehemu ya suluhisho ya upungufu wa wataalamu wa Bima ambao watakuwa sehemu ya watatuzi wa changamoto hizo ,"amesema na kuongeza

"Mamlaka ya usimamizi wa bima kama mdau muhimu tunaamini kwamba wataalamu watakaondaliwa watakuwa wanapanua wigo wa usambazaji wa huduma ya bima kwa wananchi ,uandaji wa bidhaa yakidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza idadi ya kampuni zinazotoa huduma za Bima. "Amesema Lutula

Amesema uongezaji wa wataalamu huo utasaidia pia kuongeza idadi ya wananchi watakaotumia huduma bora za bima nchini na kuweza kupata maendeleo na ninawapongeza shirika la Taifa la Bima (NIC) na Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kukubali kushirikiana na kuwa wabunifu wa kuendesha mtaala wa Bima na wanagenzi katika mfumo huu ambao utatoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza kwa nadharia watakapokua chuoni na muhula mwingine kujifunza kwa vitendo kupitia Shirika la NIC,"alisema

Aidha Lutula,alisema mfumo wa kujifunza kwa vitendo kwa wanafunzi hao utasaidia wanafunzi kuwa na uelewa mpana wa masuala ya Bima na kupata uzoefu kisha baadae kuwa mahiri katika eneo hilo la Bima na kuja kuwa msaada kwa mtu mmoja mmoja ,jamii na Taifa kwa ujumla katika eneo la biashara na uchumi.

Amesema matumaini ya Serikali na wadau Bima nchini ni kwamba mtaala huu utakidhi mahitaji ya wanafunzi ,wafanyakazi, na baadae kwaajili katika eneo la Bima kwa kuwezesha kutoa wahitimu wabunifu watakaoendana na mahitaji ya soko ndani na nje ya Tanzania .

Nae Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kama chuo wapo tayari kuwasaidia kwa chochote wanafunzi hao watakachohitaji pindi watakapomaliza elimu yao.

Amesema wahitimu hao , watumie muda huu wanapokuwa chuoni kuanza kufikilia wenyewe namna ya kujiajiri wenyewe na baadae kuja kuajili wenzao.

"Katika sekta ya bima mtakapoingia mjitume,muanze kuhakikisha mnatoa mchango katika kampuni na kujifunza na wewe utapomaliza uanze kujitegemea."Alisema na kuongeza

"Wanafunzi hawa tayari wamesoma semiter mbili kuanzia mwezi huu mwishoni wanaenda NIC watakaa miezi 14 kwa muajili na miezi 14 chuoni."Alisema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dk Elirehema Doriye alisema wao kama Shirika wanawapokea wanafunzi hao na kuwaandaa kuwa wahitimu kamili ambapo wanapotaka katika Shirika lao wanakuwa wamejifunza kikamilifu.

"Tunapompokea mwanafunzi lazima afuate maelekezo atakayopatiwa akiwa kwenye kazi tunahakikisha tunamuandaa mtu kamili ili anapotoka Chuo anaenda moja kwa moja katika ajira,"amesema Doriye

Pia amesema ni vema wanafunzi hao watakapokuwa katika mafunzo haya ya vitendo ni lazima wawe wabunifu katika sekta hiyo ya bima.
Mkurugenzi wa Ukaguzi  na Usimamizi  wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Neema Lutula akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtaala wa Bima na wanagenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akitoa maelezo namna watafavyoshirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) katika uendeshaji wa Mfumo wanangezi wanaosomea Bima katika hafla iliyofanyika kampasi ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamini Sedoyeka akizungumza kuhusiana kuanzisha kozi ya Bima katika katika hafla iliyofanyika kampasi ya Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya wanafunzi wanaosoma kozi ya Bima ya mfumo wa wanagenzi  wakiwa na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi.
Picha ya Pamoja ya menejimenti ya IAA pamoja na mgeni rasmi mara baada kuzinduzi kozi ya Bima.
Picha ya Pamoja ya wafanyakazi wa NIC na Mgeni Rasmi mara baada ya uzinduzi wa kozi ya Bima katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) katika hafla iliyofanyika kampasi ya Dar es Salaam.
Mgeni rasmi watatu kutoka kushoto Mkurugenzi wa Ukaguzi wa (TIRA)  Neema Lutula  wakiwa wameshika mtaala wa kozi wa Bima.
Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki uzinduzi wa kozi ya Bima katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Katika hafla iliyofanyika kampasi ya Dar es Salaam.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post