Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza jana na wananchi wa Kata ya Kinyeto alipofika kwenye tukio la ajali ya mtumbwi kuzama maji bwawa la Ntambuko ambapo watu wawili kati ya saba waliokuwa wameupanda kuokolewa na wengine watano kutoonekana na jitihada za kuwatafuta zikifanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza na wananchi wa Kata ya Kinyeto kwenye tukio hilo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (SACF) Ivo Ombella akizungumzia tukio hilo.
Mariam Kambi mkazi wa Kijiji cha Kinyeto akizungumzia tukio hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akipokea taarifa ya tukio hilo kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (SACF) Ivo Ombella.
Uokoaji ukiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akiwapa pole wananchi.
Wananchi wakiwa kwenye tukio hilo.
Dkt. Mahenge akisisitiza jambo katika tukio hilo.
Wananchi wakiwa kwenye tukio hilo.
Wananchi wakiwa kwenye tukio hilo.
Wananchi wakiwa kwenye tukio hilo.
Wananchi wa Kijiji cha Itamka wakiwa kwenye tukio hilo.
Wananchi wa Kijiji cha Itamka wakiwa kwenye tukio hilo.
Ndugu wa watu wanao tafutwa.baada ya ajali hiyo wakiwa na huzuni.
Ndugu wa watu wanao tafutwa.baada ya ajali hiyo wakiwa na huzuni.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kinyeto Edward Yohana akizungumzia tukio hilo.
Uokoaji ukiendelea.
Muonekano wa bwawa lilipotokea tukio hilo.
Wananchi wakiwa kwenye tukio hilo.
Ndugu wa watu wanao tafutwa.baada ya ajali hiyo wakiwa na huzuni.
Mama aliyempoteza mtoto wake Ally Hamisi ambaye ni Mwanafunzi akizungumza na waandishi wa habari.
Jitihada za kuwatafu watu hao zikiendelea kufanywa na waokoaji.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Eliya Digha akizungumzia tukio hilo.
Majonzi makubwa katika tukio hilo
Wananchi wa Kijiji cha Kinyeto wakiwa kwenye tukio hilo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida
WATU watano wakiwemo watatu wa famia moja waliokuwa wakitokea Kijiji cha Miundu kwenda Kijiji cha Kinyeto Wilaya ya Singida wanaofiwa kufa maji baada ya mtumbwi uliokuwa ukiwavusha kutoka katika kijiji hicho kwenda msibani kuzama katika bwawa la Ntambuko Kata ya Kinyeto.
Katika mtumbwi huo walikuwemo watu saba ambapo wawili kati yao akiwepo nahodha waliokolewa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Tukio hilo lililoleta simanzi kubwa kwa wananchi wa eneo hilo lilitokea jana asubuhi majira ya saa tatu.
Wanaume hao waliokuwa kwenye mtumbwi huo walikuwa wakitokea Kijiji cha Itamka Kata ya Mrama Tarafa ya Ilongero wilayani humo.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge aliyekuwepo eneo la tukio ameomba Kikosi cha Uokoaji cha Jeshi la Zimamoto kutoka Mkoa wa Manyara kwenda kuongeza nguvu ya kuwatafuta watu hao.
Mahenge alisema kazi ya kuwatafuta watu hao itafanyika usiku na mchana hadi wapatikane na kama watakuwa wamekufa miili yao izikwe kwa heshima.
"Nilikuwa Dodoma ninefika leo 'jana' asubuhi kabla sijafanya chochote nikapata taarifa hii nimekuja kuwaona na tayari nimepiga simu makao makuu ya Jeshi la Uokoaji na Zimamoto Dodoma ambapo Kamishna mkuu ametupa waokoaji wa jeshi hilo kutoka Mkoa wa Manyara ambao watafika leo hii," alisema Mahenge wakati akizungumza na wananchi eneo la tukio.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (SACF) Ivo Ombella alisema baada ya kupata taarifa hiyo walifika katika eneo hilo ambapo kazi ya kuwatafuta watu hao inaendelea chini ya waokoaji wanne.
Ombella aliwataja watu waliookolewa kwenye tukio hilo kuwa ni Jafari Adamu (30) na Musa Saidi aliyekuwa nahodha wa mtumbwi huo.
Aliwaja watu wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Ayubu Mohamed (39) Abubakar Hassani (25) Abubakar Hamisi (35) Hamisi Ali (30) na Ali Hamisi (18) ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha nne Sekondari ya Mrama.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mtumbwi huo kupigwa na mawimbi katika bwawa hilo.
Habari zilizo patikana katika tukio hilo zimeeleza kuwa wanaume hao walikuwa wakienda
nyumbani kwa Abdulahi Ramadhani kwenye msiba wa binti yao ambaye aliamua kujitoa
uhai wake baada ya mume wake kudaiwa kuoa mke wa pili.
By Mpekuzi
Post a Comment