NA Abel Paul Jeshi la Polis Mkoa wa Arusha
Tarehe 26.07.2021 waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh.George Simbachawene amefanya ziara Katika Jiji la Arusha na kukagua Maeneo mbali mbali yanayohusu Wizara yake.
Katika ziara yake Mkoa wa Arusha Mh.Simbachawene alianza kwa kutoa salaam za rambi rambi kwa familia ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Marehemu Mama Anna Mghwira ambapo amewasihi wanafamilia kumwomba Mungu awape moyo wa uvumilivu kipindi hiki kigumu
Mh.George Simbachawene alianza kwa kukagua kituo cha Polisi Utalii ambacho kinadili na maswala yote yanayohusu utalii,Jeshi la zimamoto na ukoaji,Jeshi la Magereza,Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa(NIDA) na Baadae Mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga.
Aidha amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha namna wanavyotoa huduma bora katika vituo vya utali vilivyopo jiji la Arusha Pia namna wanavyo pambana na uhalifu katika Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wa Jeshi la Magereza amelitaka kuja na mikakati ya kisasa kama kilimo cha tija kwa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla pia vifaa vya ndani ambavyo vinatengenezwa na kiwanda chao kuhakikisha Wanajitangaza.
Pamoja na hilo amekagua Jeahi la zimamoto na ukoaji ambapo amewataka kuwajibika ipasavyo na kukabiliana ajali za moto pia amewataka kuunda tume zitakazo weza kuja na majibu kuhusiana na changamoto za shule kuungua moto.
Sambamba na hilo amekagua Mpakani mwa Tanznaia na Kenya NAMANGA nakuzitaka mamalaka husika ziweke mikakati dhabiti ya kupambana na uhalifu mipakani ikiwemo na wale wanaovuka mipaka bila kufuata utaratinu za Nchi.
By Mpekuzi
Post a Comment