Hakainde Hichilema, mfanyabiashara aliyejitengenezea utajiri wake, ni kiongozi kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kupitia United Party for National Development (UPND).
Hichilema alizaliwa Juni 4, 1962 kusini mwa Monze.
Baada ya kwenda shule ya eneo alikozaliwa, alijiunga na Chuo Kikuu cha Zambia kwa ufadhili wa serikali ambapo alisoma na kuhitimu mnamo 1986 na Shahada ya Sanaa (BA) katika Uchumi na Biashara.
Baadaye alipata shahada ya uzamili ya somo la Fedha na Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza.
Tangu wakati huo, Hichilema, anayejulikana kwa upendo na jina lake la utani kama HH, ameandika rekodi ya kuvutia katika biashara, ndani na kimataifa.
Hichilema maarufu sana kibiashara, sasa ni mfugaji wa pili mkubwa wa mifugo nchini Zambia na mifugo karibu 100,000 chini ya jina lake katika mashamba yake manne, na ni mmoja wa wauzaji wakubwa wa nyama kwa soko la ndani la Zambia, na pia mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa zaidi nchini Zambia wanaouza nje ya nchi bidhaa zitokanazo na nyama ya ngombe.
Pia ana uwekezaji mkubwa katika sekta ya utalii ya Zambia.
Kufuatia elimu yake ya chuo kikuu, Hichilema alipanda katika nafasi za juu katika ulimwengu wa mashirika nchini Zambia, akipata kazi za kifahari kama Mkurugenzi wa kampuni ya Coopers na Lybrand akiwa na umri wa miaka 32, kutoka 1994 hadi 1998, na baadaye kama mrithi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Cooper, Grant Thornton, kutoka 1998 hadi 2006.
Alikuwa pia mkubwa zaidi katika kampuni mbili zinazomilikiwa na wageni ikiwa ni pamoja na Benki ya Barclays Zambia.
Aidha, Hichilema ni mtaalamu wa majadiliano ya Biashara, na ni mwanachama wa Taasisi ya Wakurugenzi ya Zambia.
Bwana HH alishinda urais wa chama cha upinzani UPND mnamo mwaka 2006 kufuatia kifo cha kiongozi wake, Anderson Mazoka, mshauri wake wa biashara ambaye pia alikuwa rafiki yake wa karibu.
Tangu wakati huo wanasiasa wa chama tawala, bila mafanikio, walikuwa wakijaribu kumuhusisha na kesi za kisheria ambazo amekataa kuziacha ziwe kuzuizi cha kufikia ndoto zake.
Katika uchaguzi mdogo wa urais wa Januari 2015, Hichilema alikuwa wa pili katika kinyanganyiro hicho nyuma ya mgombea wa chama cha PF aliyekuwa madarakani, akipungukiwa na kura 27,000 tu.
Ameendesha kampeni zake akiegemea zaidi suala la uchumi, akisema kwamba Zambia inahitaji kiongozi anayeelewa biashara na anayeweza kugeuza uchumi ili kufungua faida za maendeleo katika afya, elimu na nyanja zinginezo.
Ana shauku ya kuboresho mfumo wa elimu wa Zambia ili kila Mzambia mchanga apate fursa aliyopata ya kupokea msaada wa serikali ambao unaweza kuwawezesha vijana kuanzisha taaluma nzuri na kuwawezesha kupata mshahara mzuri, kukidhi mahitaji ya familia zao na kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa Zambia.
Na pia, Hichilema sio mwanasiasa tu na mfanyabiashara pekee, pia ni mfadhili, akichangia pakubwa shughuli za jamii na miradi kama kliniki, shule, ujenzi wa visima na kujenga mabwawa ili kuboresha shughuli za kilimo.
Amefunga pingu za maisha na Mutinta na kwa pamoja wamejaaliwa watoto watatu.
from Author
Post a Comment