Jina Kikwazo Kesi ya Sabaya |Shamteeblog.



KUKOSEWA kwa jina la tatu la mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha Lengai Ole Sabaya, kumesababisha malumbano ya kisheria na kuahirishwa kesi kwa muda.

Katika hati ya maelezo ya mashitaka, jina Sabaya limesomeka Sayaba na kusababisha kuibuka kwa malumbano ya kisheria.

Malumbano yalianza saa nne asubuhi hadi saa sita mchana baada ya upande wa Jamhuri kupitia Wakili Mwandamizi, Abdallah Chavula na Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka kuomba marekebisho madogo ya hati hiyo kutokana na kubaini makosa ya kiuchapaji.

Wakili wa serikali Abdallah Chavula ameieleza mahakama kuwa kilichotokea ni makosa ya uwandishi lakini mshtakiwa ni Lengai Ole Sabaya na si sayaba kama hati inavyoonesha


Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Chavula aliiomba mahakama kubadilisha jina la Sayaba kuwa Sabaya kupitia sheria namba 234 kifungu kidogo cha kwanza cha makosa ya jinai mwaka 2019 Sura ya 20 .

Katika kesi hiyo washitakiwa wengine ni Sylvester Nyengu na Daniel Mbura ambao majina yao yapo sawa.

Nae Wakili wa upande wa utetezi,Mosses Mahuna, akaiambia mahakama kuwa mshitakiwa uyo alikutwa na kesi ya kujibu mahakamani kwa hati iyo ya 16 July 16, 2021 na alikutwa na kesi ya kujibu baada upande wa mashtaka kufunga kesi yake na mshatiwa alianza kujitetea na wakati wa utetezi wake alianisha mapungufu hayo yaliyo katika hati ya mashtaka ambayo ilimkuta na kesi ya kujibu.


Wakili Mahuna akadai wao hawapingi mshtakiwa namba moja Lengai Ole Sabaya ila wanampinga mshtakiwa aliyeletwa katika hati ya mashtaka ambaye ni Lengai Ole Sayaba.

Mahuna akaongezea kusema kuwa suala hilo linataka kurekebishwa wakati wa mahojiano baina ya Jamhuri na mshitakiwa wakati upande wa jamhuri walileta mashahidi 11 na mawakili wasomi Wanne wa serikali kuthibitisha hati ya mashtaka yenye jina la mshtakiwa uyo Lengai Ole sayaba.

Hata hivyo, baada ya mvutano wa hoja za kisheria baina ya mawakili wa pande zote mbili juu ya marekebisho ya jina la mshtakiwa namba moja Lengai Ole Sabaya uliodumu kwa takribani saa mbili mahakama imetoa uwamuzi mdogo wa kukubali marekebisho hayo ya jina la mshtakiwa uyo Lengai Ole Sabaya kutoka kwa kwa Lengai Ole Sayaba kama inavyosomeka hati ya mashtaka na kuwa Lengai Ole Sabaya na mahakama kueleza kuwa marekebisho hayo hayatakiuka haki kwa mshtakiwa huyo,

Wakili wa upande wa mashtaka Abdallah Chavula akawasomea tena washtakiwa wote mashtaka yao huku mshatikiwa namba moja akiwa ni Lengai Ole Sabaya baada kufanyika kwa marekebisho ya jina la mwisho na washatakiwa hao wote watatu wamekana tena mashtaka hayo.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post