Maajabu !! SAMAKI MWENYE KICHWA CHA KONDOO NA MENO YA BINADAMU AKAMATWA |Shamteeblog.




Samaki mwenye kichwa cha kondoo
Samaki asiye wa kawaida mwenye meno ya binadamu amekamatwa nchini Marekani.

Picha ya samaki huyo ilisambazwa katika mtandao wa facebook .

Alitambuliwa kama samaki mwenye kichwa cha kondoo 'Sheephead fish', ambaye ana meno kama ya binadamu ya kuvunja chakula.

Samaki huyo anaonekana kupata jina hilo kutokana na mdomo wake kuwa na muonekano kama ule wa kondoo.

Samaki huyo anadaiwa alikamatwa na Nathan Martin ambaye amekuwa katika gati hiyo.

Bwana Martin alisema alikuwa na matumaini ya kumshika samaki mwenye kichwa cha kondoo wakati alipoona mdomo uliojaa meno.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post