MWIGIZAJI wa filamu nchini, Yvonne Cherrie, maarufu kwa jina la Monalisa ni miongoni mwa mastaa wa kike wanaosifika katika fani ya maigizo nchini.
Monalisa ambaye Agosti 19, 2021 ametimiza miaka 40, leo Agosti 18 (Jumatano), ameshea story kwa mashabiki wake kwamba alianza kuigiza kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 19, wakati huo akiwa anamnyonyesha binti yake Sonia aliyekuwa mtoto mchanga kabisa.
Monalisa alimpata Sonia na aliyekuwa nguli wa kutayarisha filamu nchini, George Tyson ambaye kwasasa ni Marehemu. Na filamu yake ya kwanza kuigiza ilikuwa ni ‘Girlfriend’ ambayo ilitoka mwaka 2003.
“Nilianza kujulikana na Watanzania miaka 21 iliyopita kama Muigizaji nikiwa na umri wa miaka 19 kama umri huu alionao sasa binti yangu @soniamonalisa
Haikuwa safari rahisi ya kuishi kama Monalisa kwa zaidi ya Miongo miwili kama watu wanavyodhani, lakini nashukuru kwamba nimeweza kumtenganisha Monalisa na Yvonne.
Filamu yangu ya kwanza GIRLFRIEND niliigiza huku nikiwa namnyonyesha binti huyu akiwa mchanga kabisa. Look at us now!! Twinning!!
Hakika SIKU HAZIGANDI.
Ndugu zangu rasmi naingia floor ya 4. Huwezi amini, tofauti na wanawake wengi ambao wanaogopa ukubwa, mimi nina furaha mno kuiona siku hiyo ya kesho.”amesema Monalisa kupitia page yake ya Instagram.
from Author
Post a Comment