MWALIMU AFARIKI KWA KUPIGWA SHOTI YA UMEME AKIZUNGUMZA NA SIMU HUKU AKIICHAJI |Shamteeblog.


Mwalimu wa shule ya upili ya Kimugui kaunti ya Bungoma nchini Kenya amepatikana akiwa amefariki dunia chumbani mwake baada ya kupigwa na umeme akichaji simu yake ya rununu 'Smartphone'.

Kwa mujibu wa jirani yake Mercy Wachina alisema Job Wafula alishikwa na usingizi kabla ya kuondoa chaja kwenye soketi.

"Alikuwa akizungumza kwenye simu akiichaji, alishikwa na usingizi kabla ya kuondoa chaja kwenye soketi. Wafula alipatikana siku ya Jumatano, Agosti 18,2021 akiwa amefariki dunia," Jirani yake Mercy Wachina alisema.

Wafula alikuwa mwalimu katika shule ya upili ya Kimugui eneo bunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma, pia alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton na alikuwa anasubiri kuhitimu na shahada ya ualimu.

"Marehemu alikuwa akifunza somo la Hisabati na kemia katika shule ya Kimugui," aliongezea Wachina.

Rafiki wa karibu wa marehemu Noah Wanjusi alisema kwamba simu yake ililipuka na imeharibika sana.

"Simu yake imelipuka na haifanyi kazi, hii inamaanisha alipigwa na umeme," Wanjusi alisema.

 Familia yake imepanga kufanya mchango siku ya Jumapili, Agosti 22,2021 na marehemu atapumzishwa Jumatano, Agosti 25,2021.

Chanzo - Tuko News



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post