Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wananchi na wadau wa misitu wilayani Mufindi wametakiwa kuendelea kulilinda shamba la miti la Sao Hill kwa kuwa linachangia kwa asilimia kubwa la uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na wadau wa uvunaji wa miti katika shamba hilo wapata kuwa 368,mhifadhi mkuu wa shamba la miti la Sao Hill,Lucas Sabida alisema kuwa shamba hilo limekuwa linasaidia kukuza uchumi wa wananchi kupitia malighafi za miti ambao zinapatikana hapo.
Alisema kuwa wananchi,wadau na serikali kwa ujumla wanatakiwa kuimba wimbo mmoja katika kuhakikisha kuwa walilinda shamba hilo ambao limekuwa likikuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Sabida alisema kuwa serikali itasimama kuhakikisha shamba hilo linakuwa chombo muhimu katika kutengeneza Ajira na ukuaji wa uchumi wa Wana Mufindi na Taifa kwa ujumla kwa kutegemea malighafi zote ambazo zinapatikana katika shamba hilo.
Alisema kuwa sekta ya uvunaji ni sekta inayotegemea zaidi kiuchumi hivyo ni muhimu kwa wavunaji kushirikiana na Serikali kuibua changamoto ili zipatiwe ufumbuzi katika kuchochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu.
Sabida alisema kuwa mwaka jana shamba hilo halikufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kutokana na kushuka kwa uchumi kutokana na kudorora kwa soko la mbao kutokana na mlipuko wa ugonjwa UVIKO 19.
“Kwa mwaka 2021 Wavunaji 323 Waliizinishwa kuvuna Hadi June 30 waliofanikiwa kuvuna ni 123,wengi wao walishindwa kuvuna kutokana na changamoto mbalimbali hivyo Uvunaji ulfikia asilimia 60 tu mapato ya serika bil 33.5 badala ya 55.5 changamoto kubwa ni kudorora kwa soko kutokana na Covid 19” alisema Sabida
Alisema kuwa changamoto nyingine ya wavunaji wa shamba hiyo ni wananchi kuvuna miti yao ikiwa haijafikia ubora unaotakiwa na kuuzwa kwa gharama nafuu soko tofauti na wavunaji kutoka katika shamba la Sao Hill.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi,Saad Mtambule alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wavunaji hao wanatafutiwa masoko ya mazao ya miti katika nchi za nje kama Congo na Zambia ambazo kwa kiasi kikubwa wameonyesha nia ya kuitaka bidhaa zinazotoka na zao la miti kutoka katika shamba la Sao Hill.
Alisisitiza kuwa serikali imejipanga kuakikisha kuwa inamaliza changamoto zote ambazo wavunaji hao wa zao la miti katika shamba hilo ili waendelee kuvunja na kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla.
Mtambule alisema kuwa wadau,wananchi na serikali wanatakiwa kuendelea kulilinda shamba hili na majanga ya moto ambayo yamekuwa yanarudisha nyuma juhudi zinazofanywa na uongozi wa shamba hilo.
“Nyinyi wavunaji lazima mjivunie uwepo wa shamba hili kwa kuwa linatoa zao bora kuliko mahali pengine pale hapa nchi ndio maana malighafi zake zimekuwa zinadumu kwa miaka mingi hivyo mwendeni sokoni mkiwa kifua mbele kutokana na bidhaa zenu” alisema Mtambule
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi katibu wa wavunaji wa miti katika shamba la miti la Sao Hill Dr Bazir Tweve alisema kuwa wanavunaji hao wanakabiliwa na changamoto zifuatazo bei kubwa ya malighafi,kulipia log cess kwenye standing tree,kulipia ushuru wa mbao wakati umelipiwa log Cess,kulipia VAT ya 8% kwenye standing tree na kwenye mauzo na ushuru wa mbao kwenye mageti mbalimbali na tozo nyingine nyingi.
Alisema kuwa wavunaja wamekuwa wanakumbana na changamoto ya miundombinu hasa barabara katika maeneo wanayokwenda kuvuna miti,kucheleweshwa kwa upimaji wa maeneo ambayo wavunaji wanakuwa wamepewa kuvuna miti.
Dr Tweve alimalizia kwa kuupongeza uongozi wa TFS kupitia shamba la miti la Sao Hill kwa juhudi za kulilinda shamba hilo na kutunza malighafi ambazo zinapatikana katika shamba hilo ambazo zinasaidia kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
Naye msaidi wa mhifadhi mkuu wa shamba la Sao Hill Ignas Lupala alisema kuwa wamefikia asilimia 80 ya upimaji wa maeneo ambayo wavunaji wamepewa na kuondoa changamoto hiyo,wageni hawarusiwi kuvuna miti katika shamba hili bali wanatakiwa kununua mazao kutoka kwa wavunaji wazawa.
Lupala aliwataka wavunaji kuhakikisha wanafuata sheria zote za uvunaji huku wao wakijipanga kuhakikisha wanazitatua changamoto ambazo wavunaji hao wanakabiliana nazo.
By Mpekuzi
Post a Comment