Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere unaosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania unatangaza nafasi za udhamini (Scholarships) wa masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2021/2022.
Ufadhili huu, unalenga kuongeza hamasa na ufaulu kwa wanafunzi wa kike hapa nchini katika masomo ya Hisabati na Sayansi. Unajumuisha gharama zote za ada, pesa za kujikimu (malazi na chakula), mafunzo ya vitendo na vifaa vya kujifunzia ikiwemo kompyuta mpakato (Laptop). Utatolewa kwa wanafunzi kumi (10) raia wa Tanzania wenye ufaulu wa kiwango cha juu waliosajiliwa katika vyuo vikuu vinavyotambulika nchini.
Kwa Shahada ya Kwanza, ufadhili utatolewa kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka 2021 na wenye ufaulu wa daraja la kwanza miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa, katika makundi yafuatayo:
a) Wanafunzi wa kike tu, waliochaguliwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Hisabati au Sayansi.
b) Wanafunzi wa kike na kiume, waliochaguliwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Hisabati, Sayansi, Uchumi, TEHAMA, Uhasibu au Fedha.
Orodha ya wanafunzi kumi bora itapatikana toka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Kwa Shahada ya Uzamili, ufadhili utatolewa kwa wanafunzi wa kike na kiume, wenye ufaulu wa juu katika shahada ya kwanza kujiendeleza katika fani ya Hisabati, Sayansi, Uchumi, TEHAMA, Uhasibu au Fedha Maombi yanakaribishwa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu udhamini huo na fomu za maombi <<BOFA HAPA>>
from Author
Post a Comment