************
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa viwango vya Magari yaliyotumika, Spare parts (vipuri) na gereji, dhumuni la kuandaa viwango hivi ni kuwajengea uwezo wenye gereji kuendesha shughuli zao kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuwaongeza imani kwa wateja wao ikiwa wamethibitishiwa ubora kwa kiwango husika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam Afisa Viwango TBS, Bw.Cyril Kimario amesema magari yaliyotumika yanakuwa na mifumo ambayo ikitumika kwa muda mrefu inapoteza ubora wake hivyo inahitajika kufanyiwa marekebisho katika mifumo hiyo kama vile mifumo ya breki, mifumo ya mafuta, mifumo ya taa, mifumo ya hewa na mifumo mingine.
"Hiki kiwango cha magari yaliyotumika (used motor vehicles) kimekuwa kikitumika kwa muda mrefu ambacho ni kiwango namba TZS 698 cha mwaka 2012 ambapo mawakala wetu wa ukaguzi wa magari walikuwa wanakitumia hiki kiwango kukagua magari kabla hayajaingia nchini". Amesema Bw.Kimario.
Amesema kuna kiwango kingine ambacho ni kiwango cha Spare parts TZS 1960 ambapo kinapima kwa ujumla vifaa vyote yaani vipuri (spare parts) ambapo kuna viwango vinavyoambatana navyo kama kiwango cha matairi specifics, kiwango cha spring specifics, kiwango cha taa specifics, na kiwango hiki namba TZS1960 ni kiwango cha ujumla kwa vipuri vyote.
"Ili uweze kugundua vipuri hivi (spare parts) vina ubora ni lazima kiwango hiki kitumike kupima vipuri hivyo (spare parts) na kikishaangaliwa vizuri na kinaelezea matakwa ya vipuri". Amesema.
Aidha amesema kuna kiwango kingine cha kupima gereji ambazo zinarekebisha magari yenye dosari nchini ambacho kimeandaliwa mwaka 2017 hiki kiwango si cha lazima ni kiwango cha hiari ila kinaongeza thamani pale ambao umekitumia ili kujiridhisha na gereji yako.
"Kiwango hiki kinatoa fursa kwa wamiliki wa gereji kwa ajili ya kuonesha umahiri wao wa ukarabati wa magari yenye dosari. Kiwango kinaelekeza namna ambayo gereji inatakiwa kewa na pia vifaa vinavyohitajika pamoja na mazingira yaweje kulingana na aina ya magari yanahudumiwa katika gereji hiyo". Amesema Bw.Kimario.
By Mpekuzi
Post a Comment