Na Linda Shebby
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo ametoa pongezi kwa niaba ya serikali kwa uongozi wa Clouds Media Group kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Joseph Kusaga (Big Joe) kutokana na mchango wake mkubwa wa kuisaidia serikali katika kutoa ajira kwa vijana nchini.
Profesa Mkumbo aliyasema hayo jana usiku ambapo alikua mgeni rasmi kwenye sherehe ya kuwakabidhi vijana 55 waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Mi.10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe ambapo walichujwa kutokana na michanganuo yao ya biashara ambapo vijana zaidi ya 5,000 walishiriki katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Aidha kigezo kikubwa walichishindanishwa walifanikiwa kupata mchongo huo ni kwa zile Kampuni ambazo hazikuwahi kutangaza na Clouds hata Mara moja."Clouds mna mchango mkubwa sana katika sekta ya ajira nchini wenye umri kama wangu wengi wanajua Clods walipoanzia , ikiwemo kukuza vipaji kwa vijana kwa wasanii mbalimbali nchini".
"Mimi pia nimefaidika kwa kupitia Kipindi chenu Cha 360 mlinipa nafasi ya kuja na kuzungumza mambo mbalimbali nakuja napiga maneno hapa kama wengi tunavyojua Rais wa awamu ya Tano Hayati John Joseph Magufuli alikua akiangalia sana kipindi hiki na wakati mwingine alipiga simu hivyo na Mimi mlinitengeneza sababu aliniona kupitia vipindi mbalimbali nawashukuru sana" alisema Profesa Mkumbo.
Aliongeza kwa kusema kuwa angenda ya serikali ya awamu ya sita ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuweka mazingira mazuri ya biashsra, uwekezaji na Ubunifu nchini hivyo serikali inawaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha CMG.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Goodwin Gondwe alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ambapo alitoa salaam pongezi kwa CMG kwa kutoa ajira kwa vijana na kuahidi kuendelea kufanya nao kazi bega kwa bega.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali mashuhuri, wasanii, pia walikuwepo Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa'ambaye ni msanii maarufu wa muziki wa Kizazi Kipya na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ' Nikki wa Pili'.
Wasanii wengine waliotoa burudani na kukonga wahudhuriaji wa hafla hiyo ni pamoja na Damian Soul, Jose Mara pia Mbunge Nape alipanda jukwaani na kuonesha kipaji chake cha kuomba na kukung"uta gitaa.
Naye Mkurugenzi wa CMG Joseph Kusaga ametoa wito kwa vijana waluopata bahati ya kupenya kwenye kinyang"anyiro Cha Mchongo wa Big Joe kuwa wasiwe wachoyo na kupata kwao iwe ni fursa ya kuwanyanyua vijana wengine huku akisisitiza kwamba Ubunifu ndiyo ngao katika mapambano kwenye kutafuta maisha.
Mchongo huo umekuja mwaka huu ambapo Mkurugenzi huyo wa CMG ametimiza umri wa miaka 55 hivyo akaona arudishe alicho nacho kwa jamii .
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo akizingumza na vijana pamoja na wafanyakazi wa Clouds Media Group kwenye hafla ya kuwakabidhi vijana 55 waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Milioni 10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Nape Nnauye akiwa jukwaani na kuonesha kipaji chake cha kukung"uta gitaa. hafla ya kuwakabidhi vijana 55 waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Milioni 10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Nape Nnauye akizungumza jambo kwenye hafla ya kuwakabidhi vijana 55 waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Milioni 10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye ya kuwakabidhi vijana 55 waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Milioni 10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga wakiwa kwenye picha ya pamoja na vijana 55 wakati wa hafla ya kuwakabidhi vijana hao waliofanikiwa kupata matangazo yenye thamani ya Milioni 10 kwa kupitia Mchongo wa Big Joe iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi hiyo vilivyopo Mikocheni Mkoani Dar es Salaam. Kushoto ni .
By Mpekuzi
Post a Comment