Na John Walter-Babati
Wadau wa mchezo wa riadha mkoa wa Manyara wamelalamikia kukosekana kwa njia ya kukimbilia (running truck) katika uwanja wa Kwaraa kutokana na ujenzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na uzio wa ukuta unaotenganisha shule ya msingi Babati na uwanja huo wa michezo.Wametaja ujenzi huo kama sababu inayodhoofisha mchezo wa riadha licha ya kutoa ushauri wa namna ujenzi unavyotakiwa kufanywa.
Wamesema mchezo huo licha ya kuutambulisha mkoa huo lakini haupewi kipaumbele na viongozi wa mkoa huo.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Hamisi Katimba amekiri kuaathirika kwa mchezo wa riadha na kusema kuwa ujenzi huo unaoendelea ni kutokana na kufuata maelekezo kutoka ngazi ya juu.
Naye katibu tawala wilaya ya Babati Khalfan Matipula amesema kukosekana kwa uwanja wa riadha katika wilaya hiyo inawafanya wachezaji kukimbilia mkoa jirani wa Arusha.
Katibu Tawala wilaya ya Babati Halfan Matipula amesema kuhusiana na ujenzi wa uwanja huo ni suala ambalo lipo kwa mujibu wa utaratibu wa Halmashauri ya mji kwa kushirikisha madiwani kwenye vikao ambao ndio waamuzi wa mambo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Babati Half Marathon Ali Kericho amesema viongozi kutoka ofisi ya Utamaduni na Michezo katika Halmashauri ya mji wa Babati imeshindwa kuwasemea.
Wadau hao wamesema kuhusu kujengwa kwa uwanja wa Halmashauri katika eneo la katani ni hadithi ya miaka mingi wanachotaka wao ni eneo la kufanyia mazoezi katika uwanja huo wa Kwaraa kwa kipindi hiki ambacho wanaungoja uwanja mpya.
Mdau mwingine wa riadha Inyasi Melkiori amesema hawajafurahishwa na kitendo cha halmashauri kujenga ukuta hadi katika laini za wakimbia riadha na kwamba walishampigia simu Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kumweleza suala hilo.
By Mpekuzi
Post a Comment