Waziri Dkt Gwajima Amtembelea Mtoto Aliyekuwa Anamuuguza Bibi Ake Na Kushindwa Kwenda Shule Jijini Mwanza |Shamteeblog.

 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima Mtoto Shamsa Ramadhan Yusuph (mwenye sweta ) ambaye alipatwa na changamoto ya kumuuguza Bibi yake Angelina Francis na kushindwa kwenda shule wakati alipomtembelea mtoto huyu katika shule anayosoma jijini Mwanza. (Picha  na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW)

Na Mwandishi Wetu Mwanza
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameawata Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Maendeleo ya Jamii kote nchini kushirikiana kwa karibu na wadau kuibua changamoto za Jamii na kuzitafutia ufumbuzi.

Ameyasema hayo mkoani Mwanza wakati alipomtembelea Mtoto Shamsa Ramadhan Yusuph ambaye alipatwa na changamoto ya kumuuguza Bibi yake Angelina Francis na kushindwa kwenda shule.

Waziri Dkt. Gwajima ampongeza Mmiliki wa Shule ya Awali na Msingi Eden, Charlote Mbabazi ambaye amejitolea kumsomesha na kumhudumia mtoto huyo shuleni hapo.

"Mimi nikushukuru sana umefanya suala la kizalendo sana kumsaidia mtoto huyu kwa kuhakikisha hakosi haki ya kupata elimu itakayomsaidia katika maisha yake" alisisitiza Waziri Dkt Gwajima.

Aidha Waziri Dkt Gwajima amefurahishwa na uwezo mkubwa alionao Mtoto Shamsa katika masomo yake ikwia ni muda mchache tangu apelekwe shuleni hivyo kuwataka waalimu waendelee kumsimamia na kumpa mafunzo yatayoendelea uwezo wake.

Wakati huo huo amelipongeza Shirika la Nitetee Foundation kwa kuibua suala la mtoto Shamsa kumwuguza Bibi yake na kutopelekwa Shule hivyo ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutimiza wajibu wao kwa kuwasaidia wenye shida mbalimbali na wanaohitaji msaada.

Pia Waziri Dkt. Gwajima ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutimiza matakwa ya usajili kama inavyoelekezwa katika miongozo ya uendeshaji wa kazi husika.

"Nawapa Siku 30 kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na wale wanaotoa huduma katika Makao ya watoto kuhakikisha mnakamilisha taratibu za usajili" alisema Waziri Dkt Gwajima

Vilevile, amewataka wataalam katika ngazi zote kushirikiana na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha kwamba maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata huduma stahiki.

Akiwa mkoani Mwanza Waziri Dkt. Gwajima ametembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando alikolazwa Bibi wa Shamsa, Angelina Francis na kuwataka wahudumu wa Hospitali hiyo kuendelea kumwangalia na kuhakikisha anapata huduma zote zinazohitajika.

Akizungumza na Mhe. Waziri, Bibi Angelina Francis ameshukuru kwa huduma anazozipata hospitalini hapo kwani zimemfanya apate nafuu na kupata matumaini ya kurejea katika afya njema.

Akizungumzia hali ya mgonjwa, Mtaalam wa magonjwa ya wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fridolin Mujuni amesema mgonjwa anaendelea vizuri na wameshachukua vipimo vyote ili kuchunguza na kuona Bibi Angelina anasumbiliwa na nini na kuweza kumpatia matibabu yanayostahili.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post