Waziri Gwajima awatembelea Shamsa, bibi yake, ni yule Mtoto Anayemlea Bibi yake |Shamteeblog.



Mwanza. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima leo amemtembelea mtoto Shamsa Ramadhan (9) na bibi yake, Angelina Francis anayepatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa ya Bugando.

Agosti 9 mwaka huu Gazeti la Mwananchi liliandika habari kumhusu 'Shamsa (9); mtoto anayemhudumia mgonjwa miaka 3' ambapo Serikali na wadau mbalimbali wamejitokeza kuisaidia familia ya mtoto huyo.

Shamsa ambaye sasa anaendelea na masomo katika shule binafsi ya msingi ya Eden baada ya kuandikishwa na kuanza masomo ya darasa la kwanza.

Akizungumza akiwa shuleni hapo, leo Alhamisi Agosti 20,2021 Dk Gwajima amempongeza mmiliki wa Shule hiyo, Charlotte Edward kwa kujitolea kumsomesha mtoto huyo katika elimu ya msingi.


Pia amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Frolah Lauwo kwa kujitolea kumhudumia mtoto huyo huku akimhakikishia bibi wa mtoto huyo kwamba Serikali itasimamia matibabu yake.

Wakati huo Dk Gwajima amewaagiza Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kuhakikisha wanaunda sekretarieti itakayosaidia kubaini watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika ngazi za kaya.

"Huyu mtoto na bibi yake ni mfano wa watoto wengine wengi wanaoteseka huko mitaani nawaagiza watu wa ustawi wa jamii kuhakikisha wanafuatilia kwa undani familia zenye watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi," amesema Dk Gwajima.


Akizungumzia maendeleo ya afya ya Angelina daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake hospitali ya Bugando Fridolin Mujuni amesema vipimo vya bibi huyo vimeshakamika kinachofanyika ni taratibu za kuanza matibabu.

Naye Angelina Francis ameishukuru Serikali, wadau na taasisi mbalimbali likiwemo gazeti la Mwananchi kwa kuripoti taarifa za changamoto zinazomkabili.


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post