Dar Berby Leo...Yanga au Azam Kutoka Kifua Mbele? |Shamteeblog.





DAR DERBY: Ni Yanga au Azam leo?
Ligi Kuu Tanzania Bara(NBCPremierLeague) inaendelea leo kwenye viwanja viwili tofauti huku Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ukiwakutanisha miamba wawili, Yanga na Azam.

Mchezo huo unaonekana kuwa muhimu zaidi kwa Azam yenye pointi 4 tu baada ya mechi 3 za ligi ikiwa nafasi ya 11 wakati Yanga inaongoza ikiwa na pointi 9 baada ya mechi tatu pia.

Mchezo mwingine ambao pia utachezwa Dar es Salaam ni kati wakulima wawili, walima miwa Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro wakiwa wenyeji kwenye uwanja wa Uhuru wakiwakaribisha walima zabibu, Dodoma Jiji kutoka Makao Makuu ya nchi, Dodoma.

Dodoma Jiji wamejikusanyia pointi 7 baada ya mechi 4 wakiwa nafasi ya 5 wakati Mtibwa Sugar wana pointi 2 baada ya mechi 4 wakiwa nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post