Marekani yaidhinisha chanjo ya Pfizer kwa watoto wa miaka 5-11 |Shamteeblog.





Marekani jana imeidhinisha chanjo ya Pfizer kutolewa kwa watoto wa kati ya miaka 5 hadi 11, hatua inayofungua njia kwa watoto milioni 28 kupewa chanjo hiyo hivi karibuni. 
 
Uamuzi huo unatolewa baada ya jopo la mataalamu wa ngazi za juu wanaoishauri serikali wiki hii kuiidhinisha chanjo hiyo dhidi ya COVID-19 na kuamua kwamba faida zake ni kubwa zaidi ya madhara. 
 
Pfizer pamoja na mshirika wake BioNTech walitangaza wiki hii kwamba serikali ya Marekani imenunua dozi milioni 50 za ziada, wakati ikijiandaa kuwalinda watoto ikiwa ni pamoja na wale wa chini ya miaka mitano. 
 
Taifa hilo linafuatia mataifa machache kama China, Chile, Cuba na Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo yanatoa chanjo kwa watoto wadogo
 



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post