Msichana Aliyemuua Mama yake Mzazi na Kuutelekeza Mwili Kwenye Buti la Gari Aachiwa Huru |Shamteeblog.



Mwanamama Heather Mack raia wa Marekani ambaye alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 10 jela nchini Indonesia kwa kosa la kumuua mama yake akishirikiana na mpenzi wake, ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani.


Heather alihukumiwa mwaka 2005 na mpenzi wake Tommy Schaefer alihukumiwa miaka 18 kwa kosa la kumuua kisha kuutia mwili wa marehemu kwenye begi kisha kuutelekeza mwili kwenye Buti ya taxi, St Regis Bali hotel.



Heather na mama yake walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na mara kadhaa askari polisi waliwasuluhisha hadi alipoamua kumuondoa uhai kabisa akishirikiana msaada na mpenzi wake huyo.


Heather amesamehewa kifungo chake kilichosalia baada ya kupunguziwa kifungo cha miezi 34 kutokana na kuonesha tabia njema gerezani na sasa atasafirihwa kutoka Indonesia kurejeshwa kwao Marekani.




from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post