KAMPUNI ya uuzaji na usambazaji wa Petroli na Dizeli hapa nchini ya Vivo Energy wakishirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabani imeadhimisha wiki ya Usalama kwa kukusanya maoni na shuhuda zao za jinsi kanuni na taratibu za usalama zilizopo zinavyochangia mafanikio katika biashara.
Akizungumza na wadau na watumiaji wa Petroli na dizeli hapa nchini Kiongozi wa Health, Safety, Seculity, Environment and Quality (HSSEQ), Vivo Energy, Grant Bairstow amesema kuwa shuhuda zaidi ya 1200 zilizotolewa zikigusa mazingira, afya, bidhaa bora, ushindani, usalama na ulinzi wa watumiaji.
Kila mwaka kampuni ya Vivo Energy inaadhimisha wiki ya usalama ikiwa na lengo la kuhamasisha wafanyakazi na washirika mbambali juu ya umuhimu wa usalama wa mazingira, barabara na afya yaani HSSEQ (Health, Safety, Security, Environment & Quality).
Amsema kuwa Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni, 'UWEZO+ UTAYARI = USALAMA'.
Hata hivyo ametoa Mifano na shuhuda zilizoongoza kwa uboreshaji wa usalama kwenye makundi yote.
Amesema kuwa makundi yote yalichukuliwa na kusambazwa kwenye kampuni nzima ya VIVO Energy kwaajili ya kuhamasisha wengine kuiga mfano wa zoezi la utunzaji wa Mazingira.
“Usalama ndo kitovu cha biashara na mafanikio yetu kwa muda mrefu hapa Afrika. Nina Furaha kutoa ripoti ya kwamba tunaendelea kufanya vizuri kwa kuzingatia yote yaliyo muhimu kwetu kupitia HSSEQ kwa mwaka huu.” Amesema Bairstow
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, Khady Sene amesema kuwa lengo kuendeleza utamaduni wa kujali usalama katika maeneo yote ya biashara.“Lengo letu ni kuendeleza utamaduni wa kujali usalama katika maeneo yote ya biashara." Amesema
Hata ameelezea kuwa kwa Mwaka huu Vivo Energy Tanzania imeshirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabani katika kutoa elimu kwa madereva pikipiki pamoja na utoaji wa viakisi mwanga (reflector jacket) katika vituo 10 jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa maeneo hayo ni Mwembe yanga, Vijibweni, Kipunguni, Pugu, Goba, Mikocheni, Masaki, Ubungo, Mbezi Beach na Bunju.
Amesema kuwa VIVO Energy inazidi kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo yake ya HSSEQ ili kupata matokeo chanya na endelevu sambamba na shabaha yake ya kuwa kampuni inayoheshimika zaidi Afrika katika sekta ya nishati.
By Mpekuzi
Post a Comment