WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KUFANYIKA KITAIFA JIJINI ARUSHA |Shamteeblog.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masjo

Na.Vero Ignatus,Arusha

Maadhimisho ya siku ya nenda kwa Usalama barabarani ,yanatarajiwa kufanyika Kitaifa Jijini ARUSHA novemba 11-20, katika viwanja vya shekh Amri Abeid ambayo  yamebeba kauli mbiu isemayo ''Jali maisha yako na ya wengine barabarani''

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari   Oktoba 19,2021 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema wanatarajia mgeni rasmi  kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amewaomba  wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo, ili kujifunza na kupata elimu pamoja na kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri.

"Natumia fursa hii kuwajulisha kuwa, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limeteuwa mkoa wetu wa Arusha kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa,hivyo nawaalika wananchi kujitokeza kwa wingi.alisema Masejo

Masejo Alisema kuwa Katika wiki hiyo ya  Maadhimisho , kutakuwa na utoaji wa Elimu na ukaguzi madhubuti wa vyombo vya moto barabarani, katika uwanja wa maonesho wa Sheikh Amri Abeid ,katika  maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha na viunga vyake.

Amesema pia kutakuwa na mabanda ya wadau mbalimbali ya maonesho yatakayoelimisha na kutoa huduma mbalimbali kama vile Banda la Jeshi la Polisi, TIRA, LATRA, RSA, FIRE, AFYA,RED CROSS,ROTARY CLUB,VETA wengine wengi wanaoendelea kujitokeza na kusajiliwa kushiriki maonesho hayo kwenye maadhimisho. 

Hivyo katika siku hiyo wanatarajia viongozi mbalimbali wa kitaifa kuhudhuria,ambapo tarifa zaidi zitatolewa Kama itakavyopangwa na kamati ya maandalizi. 

"Watu wote mnakaribishwa kuhudhuria na kushiriki kujumuika nasi katika maandalizi hadi kilele cha maadhimisho haya. Niwaombe walio tayari kushiriki nasi katika maonesho hayo kama vile Taasisi za serikali na za binafsi kuwasiliana na katibu mtendaji au mkuu wa usalama barabarani (RTO) wa mkoa wa Arusha",alisema Masejo.

Kutokana na kwamba jukumu kubwa la Jeshi la polisi ni kulinda Raia na Mali zao, Jeshi la Polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limekuwa na mpango mkakati wa kutekeleza majukumu yake katika maeneo ya Utoaji wa Elimu, kufanya Operesheni na kusimamia sheria za usalama barabarani.

 "Utaratibu huu ni endelevu kwa nchi nzima ambapo ukaguzi wa vyombo vya moto na utoaji Elimu huchagiza Jeshi la Polisi kuadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kitaifa ambayo ufanyika kila mwaka katika maeneo tofauti tofauti",ameongeza.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post