Mamlaka za afya nchini Tanzania jana zimeonya uwezekano wa kuongezeka kwa kesi za COVID-19 wakati kipindi cha sikukuu kinapokaribia.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Dr. Dorothy Gwajima amesema, watu wanapaswa kuendelea kuzingatia hatua za kinga dhidi ya virusi hivyo, kwani takwimu zinaonyesha kuongezeka kwa janga hilo.
Gwajima amesema hayo katika uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya kupata chanjo ya COVID-19 iliyofanyika mjini Arusha, ambayo inalenga kutoa chanjo kwa watu kati ya 80,000 na 100,000 kila siku.
from Author
Post a Comment