Bei mpya ya petroli hii hapa |Shamteeblog.



Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kupanda kwa bei za mafuta zilizoanza kutumika leo ambapo bei ya lita moja ya mafuta ya Petroli imepungua kwa Sh9, Diseli kwa Sh67 huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh99 ikilinganishwa na bei zilizoanzia Disemba mwaka jana.

 Hii inamaanisha kwamba, mtumiaji wa bidhaa hiyo iliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, sasa atakuwa na unafuu katika kila lita moja atakyonunua.

Mkurugezi Mkuu wa Ewura, Mhandisi Godfrey Chibulunje  amefafanua  kuwa bei za mafuta zingepungua zaidi iwapo thamani ya dola za Kimarekani isingeongezeka dhidi ya Shilingi ya Tanzania. “Dola imenunuliwa kwa Sh2314.23 ikiwa ni ongezeko la thamani kwa asilimia moja,”alisema.

 Chibulunje aliongeza kuwa iwapo serikali isingepunguza tozo za taasisi pamoja na kuahirisha ukusanyaji wa ada ya mafuta Petroli ingepanda kwa kiwango cha juu cha Sh2638 kwa Dar es Salaam, Sh2648 kwa Tanga na Mtwara ingefikia Sh 2693 kwa lita.

 “Maamuzi haya yamesaidia kupunguza bei ya mafuta kati ya Sh23 na 31 kwa lita kutegemea aina ya mafuta na bandari yalipopokelewa mafuta hayo,”alisema.

 Kwa bandari ya Tanga, Petroli itapungua kwa Sh4 na Dizeli kwa Sh67 huku Mtwara Petroli ikishuka kwa Sh35 wakati Dizeli ikiongezeka kwa Sh2.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post