Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga mara baada ya kuwasili katika ofisi kwake Januari 03, 2022, kushoto ni Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussy Khamis Debe. Naibu Waziri anatarajia kuwa na ziara kukagua na kuona utekelezaji wa shughuli za Watu wenye Ulemavu Unguja na Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed akieleza jitihada za Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga mara baada ya kuwasili katika ofisi kwake Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu)Mhe. Ummy Nderiananga akiteta jambo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Thabit Idarous Faina ofisi kwake zanzibar mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akieleza mikakati ya Serikali kuongeza vyuo vya watu wenye ulemavu pamoja na kukarabati alipokuwa akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed (hayupo pichani).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu)Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussy Khamis Debe pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo Bi.Salma Haji mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga mara baada ya kuwasili katika ofisi kwake hii leo Januari 03, 2022.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussy Khamis Debe akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu Zanzibar wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussy Khamis Debe (kushoto).
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
*******************************
MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vyuo ili kuendelea kutatua changamoto wanazokutana nazo.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt. Khalid Salum Mohamed alipomtembelea ofisini kwake Januari 03, 2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kujionea shughuli za watu wenye ulemavu katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Naibu Ummy alibainisha kuwa, tayari serikali imetoa kiasi cha shilingi za kitanzania billion 8 kwa lengo ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ukarabati wa majengo chakavu ya kundi hilo nchini.
“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha masuala ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa ambapo ametoa shilingi bilioni 8 kwa ajili Ujenzi wa vyuo vipya viwili na ukarabati wa vyuo sita vya watu wenye ulemavu ili waweze kupata ujuzi kupitia elimu watakayopata na kuyafikia malengo yao”.alisisitiza Naibu Waziri Ummy
Aidha mikakati mingini ni pamoja na kuendelea kutoa vifaa saidizi kwa watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kuhakikisha miundombinu inakuwa rafiki katika maeneo yanayowazunguka ili kuwapa nafasi ya kushiri vyema katika shughuli zao za kila siku.
“Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha, kuwawezesha vifaa saidizi, kuboresha miundombinu mbalimbali ili kuendana na hali zao pamoja na kuhakikisha haki na usawa kwa watu wenye ulemavu vinapewa kipaumbele kwa kuzingatia sheria ya watu wenye ulemavu Namba 9 ya Mwaka 2010,”alisema
Hata hivyo naibu Waziri Ummy alimhakikishia Dkt. Salim kuwa wataendelea kudumisha ushirikiano baina yao kwa lengo la kuendeleza jitihada za kuwahumia watu wenye ulemavu nchini.
“Watu wenye ulemavu waliopo Zanzibar na Bara ni kitu kimoja hata mazingira ya changamoto zao zinawiana ni vyema kuitumia fursa ya kuendelea kuzitatua changamoto hizo huku tukidumisha ushirikino,”alisisitiza
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi (SMZ) Dkt. Khalid Salum Mohamed alieleza kuwa, wamendelea kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu ikiwemo uwezeshwaji kiuchumi, upatikanaji wa elimu jumuishi pamoja na kuwajengea uwezo ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
“Kipekee nikupongeze kutenga muda wako kufika Zanzibar hii ni faraja kwa kuzingatia umuhimu wa masuala yanayowahusu watu weye ulemavu, tutaendelea kuboresha mshikamano ya kiutendaji baina yetu ili kuunga mkono juhudi za viongozi wetu,”alisema Dkt. Khalid
By Mpekuzi
Post a Comment