Rais Samia amemtaka Mkuu Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Gaguti kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wore mahali pema peponi, Amina.
Rais Sarnia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama wa barabarani kuongeza juhudi za kudhibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka, na pia amewaasa madereva kufuata na kuzingatia Sheria za usalama barabarani.
By Mpekuzi
Post a Comment