Adeladius Makwega-DODOMA
Watanzania wametakiwa kutokulipiziana visasi wenyewe kwa wenyewe pale wanapokeseana huku wakitangazana baada ya kukoseana kwani kitendo hicho hakiwezi kuleta amani bali kuchochea chuki, hasira na vurugu katika jamii yetu.
Kauli hiyo imetolewa na Padri Paul Mapalala, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Imakulata ya Chamwino Ikulu, Jimbo Katoliki la Dodoma wakati wa misa ya pili ya Jumapili ya Februari 20, 2022.
“Tumeshindwa kuwasemehe wale wanaotukusea, tutambue kuwa yule ambaye hajui kusamehe hajui kupenda, mambo haya yote yanafanyika katika ngazi ya familia zetu, katika mataifa yetu na duniani kote.”
Kisasi hakijengi bali kinaharibu, unasikia huyu ni mzuri, huyu ni mbaya, hata kama mtu akikukosea msimtangaze, muite mzungumze msameheane kinyume chake ni sawa na kuweka mafuta ya taa katika moto uliokuwa unaofuka moshi, tunapaswa kupendane kwa moyo na si kwa mdomo aliongeza kiongozi huyo wa dini.
Padri Mapalala alisema kuwa wanadamu wana jukumu kubwa la kupendana na kusamehe kwani hii ni sifa moja ya Mungu wetu kwani hutusamehe wote tunaomkosea. Lakini je tunafanya hivyo? Aliuliza Paroko huyo wa Parokia ya Chamwino Ikulu.
Kandoni mwa misa hiyo iliambatana na zoezi la uchangiaji wa damu, mara baada ya misa kwisha waumini wa kanisa hilo walijitokeza kuchangia damu ambapo Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Chamwino Dkt. Philipo Ndovango akilisimamia zoezi hilo.
Akizungumza wakati wa zoezi la uchangia wa damu, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho alisema kuwa zoezi la uchangiaji damu linafanyika kila baada ya miezi mitatu katika taasisi za dini zikiwamo makanisa na misikiti na taasisi za elimu.
“Huduma ya damu kwa mgonjwa yoyote yule akifika katika kituo chatu cha Afya anapatiwa damu bure, kwani huduma huwa ni kwanza, huku kwa mwezi mmoja akinamama zaidi 160 hujifungua na kukiwa na benki ya damu.” Alibainisha kiongozi huyo wa afya katika kata ya Chamwino Ikulu, Wilaya Chamwino na mkoani Dodoma.
By Mpekuzi
Post a Comment