RC HAPI CHUPUCHUPU KUFYATULIWA...RAIS SAMIA AGEUKA MBOGO VIONGOZI WOTE WA MARA MTEGONI |Shamteeblog.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara Dkt. Ridhiwani Said kuhusu maendeleo ya utoaji wa huduma, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini Mkoani Mara leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
****


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi, Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Mara wajitathmini kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao huku akiagiza watu wote waliohusika na ujenzi wa mradi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Bunda vijijini kukaa pembeni kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo rushwa hali iliyosababisha kukwama kwa mradi huo.


Rais Samia ametoa maagizo hayo mjini Musoma leo Jumapili Februari 6, 2022 baada kupokea taarifa mbalimbali juu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo mkoa wa Mara akisema inasikitisha kuona miradi mingi ya maendeleo inashindwa kukamilika kwa wakati huku kukiwa na uongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya.


"Mkuu wa mkoa ni kama uliota maana leo nilikuwa nimepanga nikufyatue hapa hapa bahati yako umeeleza matatizo haya ya kukwama kwa maendeleo ina maana unafanya kazi na matatizo haya unayajua na umenoyesha umechukua hatua gani una bahati", amesema Rais Samia.


Amesema matatizo ya kukwama kwa maendeleo ya mkoa wa Mara yanasababishwa na viongozi waliopo ambao amedai kuwa ni wabinafsi na wabadhirifu hivyo kuwataka viongozi hao kujitathmini na kwamba suala la utendaji kazi wa viongozi hao anakwenda kulifanyia kazi na maamuzi atayatoa baada ya watu wake kufanya uchunguzi.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post