MWENYEKITI Wa Chama cha Mapinduzi(CCM,) Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba amewataka wanafunzi wa chuo cha Furahika Education College kuzingatia nidhamu na kujituma ili kujijenga kiuchumi na kutimiza malengo yao.
Akizungumza katika mahafali ya tisa ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Bi. Kate Kamba amesema chuo hicho kinaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu bora itakayowakwamua kiuchumi.
Amesema, Maarifa yanayotolewa na chuo hicho ikiwemo mafunzo ya hoteli, ufundi na sanaa Yana fursa kubwa na kuwataka kujituma na kuzingatia nidhamu.
"Nimesikia hapa chuo kinawatafutia fursa za mafunzo, mkajitume na sio kutumwa...Nitakuwa mshirika wa chuo hiki katika kuhakikisha vijana wengi wanapata mafunzo haya." Amesema.
Pia Bi. Kamba amesema katika kuboresha sekta ya elimu Serikali imetoa shilingi Trilioni 1.3 kwa ajili ya kujenga madarasa na kwa Mkoa wa Dar es Salaam madarasa 947 yamejengwa.
"Chuo hiki kipo chini ya VETA na mafunzo yanayotolewa yana tija kwa jamii, niwasihi mkuze sekta ya utalii ili ikifika 2025 tufikie lengo la kufikia milioni 10." Amesema.
Aidha ametumia wasaa hao kuwataka wananchi kushiriki kwa karibu zaidi katika mchakato wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu nchini kote.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho David Msuya amesema, wanafunzi 23 wamehitimu mafunzo hayo katika kozi mbalimbali ikiwemo hoteli, ushonaji, sanaa, mapambo na muziki huku changamoto kubwa ikiwa ni ukosefu wa taulo za kike na uhaba na ubovu wa kompyuta.
"Tunatoa mafunzo haya kwa wanafunzi wa kike waliofeli darasa la saba na walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali....Tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia watoto wetu taulo za kike ili waweze kujisitiri wakati wa hedhi." Amesema.
Chuo hicho kinatoa mafunzo ya ufundi bure kwa wanafunzi wakike walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali ili kuwajenga kiuchumi na kutimiza malengo yao.
Mkuu wa chuo cha Furahika Education College David Msuya akizungumza wakati wa mahafali hayo na kueleza kuwa wanahitaji mkono wa wadau katika suala la taulo za kike kwa mabinti wanaosoma katika chuo hicho.
Matukio katika picha katika mahafali ya tisa ya chuo hicho.
By Mpekuzi
Post a Comment