IKIWA ni Wiki ya Saba tangu kuanza kwa Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ jumla ya shilingi milioni 70 zimetolewa kwa wateja walioshinda katika droo ya kila wiki, yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya kadi katika kufanya manunuzi mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya saba ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’, Afisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Lightness Zablon amesema anawashukuru wateja kwa sababu wameona mwitikio mkubwa katika kampeni hii yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya kutumia ‘Cash’ katika kufanya manunuzi mbalimbali hasa katika vituo vya mafuta na maduka makubwa.
Benki ya NMB imeendelea kuwasisitiza wateja wake kuendeleza matumizi ya kadi zao za MasterCard kufanya manunuzi kwa kulipia kutumia Masterpass QR, Vituo vya Mauzo (PoS) au mtandaoni ili kuweza kujipatia nafasi ya kuwa washindi wa kila Wiki, kwa Mwezi, lakini pia wanaweza kushinda katika Grand Final ambapo kutakuwa na washindi 30 ambao kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu.
Drop hii ilisamimwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (GBT), Elibariki Sengasenga, ili kuhakikisha droo hizi za bahati nasibu zinafuata sheria na taratibu kuwapata washindi, na kuipongeza Benki ya NMB kwa kuwa washirika wazuri toka mwanzo wa kampeni hii ya MastaBata baada ya kufanya droo nyingi bila tatizo lolote.
Kufikia sasa, kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa Desemba mwaka jana, imeshatoa zawadi za pesa taslimu kiasi cha Sh. Mil. 95 kwa wateja 725, ambazo ni kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200, zitakazotolewa kwa wateja 1,080 katika kipindi cha wiki 10 za kampeni hiyo, inayofanyika kwa msimu wa tatu. Fainali ya NMB MastaBata itafanyika Machi mwaka huu.
By Mpekuzi
Post a Comment