WCF YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA |Shamteeblog.




Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (kushoto), akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Mfuko wakati wa semina ya siku moja kwa watendaji wa Mahakama Tanzania mjini Morogoro.
 

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO.
MCHAKATO wa malipo ya Fidia kwa wategemezi wa Mfanyakazi aliyefariki kutokana na kazi unategemea sana Mahakama, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma amesema.
Dkt. Mduma ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo ya siku moja kwa watendaji wa Mahakama ya Tanzania ili kuwajengea uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na WCF pamoja na kujenga mahusiano ya kikazi.
"Kwa namna ya pekee, mafunzo haya ni muhimu sana kutokana na nafasi yenu katika kufanikisha upatikanaji wa nyaraka mbalimbali za mirathi ambazo ndizo hutumiwa na Mfuko katika kuanzisha mchakato wa malipo ya fidia kwa wategemezi wa mfanyakazi pale mfanyakazi huyo anapofariki kutokana na ajali au ugonjwa unaotokana na kazi ", alifafanua Dkt. Mduma.
Alisema moja ya changamoto ambazo Mfuko unazifanyia kazi ni upatikanaji nyaraka kwa wakati kutoka kwa wategemezi, wasimamizi wa mirathi au ndugu wa Mfanyakazi aliyefariki sababu ya uelewa wa taratibu sahihi za kufuata hususan nyaraka zinazohitajika katika ulipaji wa fidia.
“Kupitia mafunzo haya tunatarajia mtakuwa mabalozi wazuri hususan katika kuwaelimisha wasimamizi wa mirathi, ndugu ama wategemezi wa marehemu mnaokutana nao wakati wa kuendesha mashauri ya mirathi na hivyo kupunguza changamoto hii kwa kiasi kikubwa.” Alisema.
Ameongeza kuwa semina hiyo itawawezesha watendaji hao wa Mahakama kuelewa zaidi Sheria iliyounda Mfuko wa Fidia, Mafao yanayotolewa, hatua za kufuata wakati wa kuwasilisha madai, nyaraka zinazohitajika pamoja na namna Mfuko unavyofanya tathmini za madai na kukokotoa fidia kwa mfanyakazi aliyeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi".
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Temeke, Jaji Ilvin Mugeta ameipongeza WCF kwa kuwaandalia mafunzo hayo kwani Mahakama inafanya kazi zake kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali WCF ikiwemo.
“Hivyo tunafarijika tunapopata fursa ya kuongeza uelewa wa mambo mbalimbali vilevile ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yataleta manufaa makubwa ikiwemo kuimarisha mahusiano kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchangia kukuza uchumi wa nchi yetu".
Semina hiyo iliyoshirikisha mahakimu wakazi zaidi ya 60 wa Mahakama kutoka mikoa mbalimbali nchini imefanyika Februari 14, 2022 mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akizungumza na watendaji wa Mahakama Tanzania wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko iliyofanyika mkoani Morogoro Februari 14, 2022.



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kituo Jumuishi, Temeke jijini Dar es Salaam Mhe. Jaji Ilvin Mugeta.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi, Temeke jijini Dar es Salaam, Bi. Mary Moyo, akichangia mada wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma na kulia ni Jaji Mfadwidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kituo Jumuishi, Temeke jijini Dar es Salaam, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta.

Mkurugenzi wa Uendeshaji, WCF, Bw. Anselim Peter.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, WCF. Dkt. Abdusalaam Omar

Mkuu wa Kitengo cha Sheria, WCF, Bw. Abraham Siyovelwa

Washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo.
Mmoja wa washiriki akizungumza.


Meneja Madai Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.

Picha ya pamoja




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post