Na Rahma Khamis Maelezo
Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar imepokea msaada wa wa vifaa tiba ya mama na mtoto vyenye thamani ya Tsh milioni 92 kwa lengo la kuimarisha afya bora nchini.
Akipokea msaada huo huko Wizara ya Afya, Mnazimmoja Waziri wa Wizara hiyo Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema vifaa hivyo vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba uliopo katika Hospitali za Unguja na Pemba.
Amesema ukosefu wa vifaa tiba ni jambo linalodhoretesha matibabu hasa kwa akina mama na mtoto hivyo kupatikana kwa vifaaa hivyo ni jambo jema ambalo litaweza kusaidia jamii.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa, Waziri Mazrui amefahamisha kuwa kwa sasa dawa zilizopo hazitoshelezi kutokana na wingi wa wagonjwa lakini wanafanya jitihada zaidi kuhakikisha wananchi wanapatiwa matibabu ya uhakika.
“Upatikanaji wa dawa hazitoshelezi kutokana na ongezeko la wagonjwa lakini tunajitahidi tuhakikishe wananchi wetu wanapata dawa angalau kwa kiasi kilichopo,” alisema Waziri .
Hata hivyo kwa Niaba ya Serikali Waziri huyo ameishukuru Taasisi ya PhamAcces Faundation kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuimarisha afya katika jamiii.
Nae Mkurugenzi wa PhamAcces Faundation Dkt Heri Marwa amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto katika jamii.
Aidha amefahamisha kuwa wameamua kutoa msaada huo baada ya kufanya utafiti kwa kutumia data kupitia hospitali mbalimbali Unguja na Pemba na kugundua kuwa ipo haja ya kuongeza nguvu hasa kwa akina mama na watoto.
Msaada huo umejumuisha vifaa mbalimbali ikiwemo Delivery bed, BP machine digital,Digital thamometer, Heumaque machine,hospital Screen na Examination machine.
Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mzrui (kushoto) akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Taasisi ya Pharm access Foudation ambavyo vitasaidia kutoa huduma za afya kwa mama na mtoto katika Hospitali za Wilaya ya Kaskazini “A” na Wilaya ya Micheweni Pemba,huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mzrui akitoa neno la Shukrani kwa Taasisi ya Pharm access Foundation mara baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba vitakavyosaidia kutoa huduma za afya kwa mama na mtoto katika Hospitali za Wilaya ya Kaskazini “A” na Wilaya ya Micheweni Pemba,hafla ya makabidhiano ilifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.Mkurugenzi Taasisi ya Pharm access Foundation Dr. Heri Marwa akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Vifaa tiba iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.
By Mpekuzi
Post a Comment