Na.Khadija Seif, Michuzi TV
WAMILIKI wa vyombo vya Habari washauriwa kuboresha Mifumo na kuongeza ubunifu Ili waweze kufanya kazi na Makampuni mbalimbali.
Akizungumza na Michuzi TV wakati wa kufungua Semina ambayo imewajumuisha Taasisi mbalimbali Pamoja na waamiliki wa vyombo vya Habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Blanq Amin Swai amesema ni wakati wa wamiliki wa vyombo vya Habari kuongeza ubunifu Ili kuendana na Kasi iliyopo na Kufahamu jamii inahitaji Mfumo upi.
Hata hivyo Swai, ameeleza Kwa jinsi gani Masoko mapya yanavokuja Kwa Kasi hususani Soko la Wanawake pamoja na wapambanaji na Wafanyabiashara wadogo wadogo.
Aidha ametoa wito Kwa Waandishi Wahabari Kwa namna gani waweze kuhabarisha jamii katika habari za Majanga na Matukio ya kutisha ili waweze kutoa ushauri kwa jinsi gani msaada unaweza tolewa kwa wakati huo kwenye janga hilo.
Baadhi ya wawakilishi na wadau wa vyombo vya Habari wakisikiliza Kwa makini taarifa inayowasilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Blanq nchini Amin Swai wakati wa semina. iliyoandaliwa na internews jijini Dar es salaam.
By Mpekuzi
Post a Comment