Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema sare yao ya 0-0 dhidi ya Palace ni sehemu ya mchezo, ingawa malengo yao yalikuwa kushinda.
Sare hiyo ni kicheko kwa Liverpool, ambao ni washindani wao wa karibu katika mbio za ubingwa wa EPL.
Liverpool , baada ya kuwafunga Brighton Jumamosi, waliweka tofauti ya pointi 4 tu na Manchester City.
Na endapo Liverpool watashinda katika mechi yao ya kesho dhidi ya Arsenal, basi wataweka tofauti ya alama moja tu na City.
” Nimeridhika na kilichotokea, nimeridhika pia na nafasi tuliyopo katika mbio zetu za kugombea ubingwa,” amesema Guardiola.
“Kiukweli, tumecheza vizuri na kutengeneza nafasi, lakini hatukuzitumia ipasavyo, wakati mwingine inatokea,” amesema bosi huyo wa Man City.
City walifanya jumla ya mashambulizi 18 na walimiliki mechi hiyo kwa asilimia 74.
Licha ya kugawana pointi na Palace, Guardiola bado anajipa natumaini.
” Bado kuna mechi ambazo tunapaswa kushinda, ila kwa jinsi tulivyopambana leo, sijutii,” amesema.
Amesema kwa sababu ya uzuri wa Palace, ilibidi wacheze mechi hiyo kama vile fainali.
City walipoteza nafasi kadha za kufunga wakati Mahrez alipochanja mbuga na kuingia katikati, lakini shuti lake lilienda juu.
City walifanya kila wanaloweza, lakini siku haikuwa yao.
Kipa wa Palace, Guaita alikuwa kikwazo kwa City baada ya kuokoa hatari nyingine kutoka kwa Mahrez.
Kosa kosa za City ziliendelea kumtesa Guardiola, baada ya Palace kuweka ugumu golini kwao.

The post Vita ya Man City na Liverpool yafikia patamu first appeared on KITENGE BLOG.
The post Vita ya Man City na Liverpool yafikia patamu appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment