Baadhi ya Wananchi wa Ukraine wameanza kuzisambaza video za Wanajeshi wa Urusi walioshikwa ndani ya ardhi ya Ukraine zinayoonesha Vijana wadogo waliojiunga na Jeshi la Russia wakiongea na kusema walilazimika kuingia vitani kwa kufuata amri ya Viongozi wao lakini sio kwa mapenzi yao.
Video hii ambayo imeoneshwa na UATV mmoja wa Wanajeshi hao wamesema waliamshwa usiku na kuwambiwa kuhusu kuvuka mpaka na kuivamia Ukraine na kwamba wakati wanasogezwa mpakani waliambiwa wanakwenda kulinda amani.
"Msafara wetu ulishambuliwa, miguu yangu imevunjika na nimepata msaada mzuri hapa, hamna haja ya Wanajeshi wengine kuja Ukraine..." amesema mmoja wa Wanajeshi hao.
from Author
Post a Comment