Airtel yakabidhi gari kwa mshindi wa promosheni ya Tesa Kimilionea |Shamteeblog.


Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania leo imekabidhi gari mpya aina IST kwa mshindi wa kwanza wa kubwa ya Tesa Kimilionea. Kwenye promosheni ya Tesa Kimilionea, Airtel imekuwa ikitoa fedha taslimu Tzs 100,000 kwa washindi 100 pamoja na Tzs 1,000,000 kwa kila wiki huku kwenye droo kubwa ambayo inachezwa kila mwisho wa mwezi washindi wawili ushinda Tzs 10,000,000 na mwingine gari mpya aina ya Toyota IST.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo ya gari mpya aina ya Toyota IST kwa mshindi huyo ambaye ni Mchite Mchite mkazi wa Mbangala jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alimpogeza kwa kuwa mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari kwenye promosheni ya Airtel Tesa Kimilionea.

‘Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mshindi wetu wa kwanza kwa kujishindia zawadi ya gari aina ya IST kwenye promosheni hii ya Tesa Kimilionea. Hii ni promosheni maalum kwa wateja pamoja na Mawakala wa Airtel wanafanya miamala mbali mbali kwa kutumia Airtel Money kuweza kuwa mshindi. Kwa nawaomba wateja pamoja na wakala wa Airtel Money kutambua kwamba kila unapofanya muamala wowote kwa kutumia Airtel Money basi unaingia moja kwa moja kwenye droo na hivyo kuwa kwenye ya kujishindia zawadi mbali mbali kama Tzs 100,000, Tzs 1,000,000 kwa droo ya wiki na zawadi kubwa ya Tzs 10,000,000 au gari mpya aina ya IST kwa kila mwezi’.

Na kama tulivyomsikia mshindi wetu hapa kama alivyosema kuwa mteja au wakala wa Airtel Money haitaji kulipia chochote au kujisajili ili kuingia kwenye droo ya Tesa Kimilionea. Vile vile, unapokuwa mshindi hakuna kulipia chochote ili kupata zawadi yako. Alisema Mmbando huku akiongeza kuwa mshindi atapigiwa simu kwa kutumia namba ya huduma kwa wateja ya +255 100 na sio vinginevyo.

Kwa upande wake, mshindi huo Mchite Mchite mara baada ya kukabidhiwa gari lake mpya aina ya Toyota IST aliwashukuru sana Airtel Tanzania kwa kuweza kuleta huduma bunifu na nafuu kwa wateja ambazo leo zimemuwezesha kuweza kujishindia gari. ‘Naomba kutoa pongezi dhati kwa kampuni ya Airtel kwa promosheni hii ambayo leo mimi mwenyewe nimeweza kujishindia gari. Ni kweli kwamba mteja au wakala haitaji kujisajili au kulipia chochote ili kuweza kuwa mshindi. Mimi nilikuwa nafanya tu miamala mbali mbali kwa kutumia Airtel Money na hatimaye nikapigiwa simu kuwa mimi ni mshindi wa gari. Nilikuwa siamini kama ni kweli mpaka nilipokuja hapa na kuonyesha gari langu, alisema Mchite.

Naomba nitoe rai kwa wateja na mawakala wa Airtel kuendelea kutumia huduma za Airtel Money kwani kila mtu anaweza kuwa mshindi. Kama mimi nimeweza kujishindia gari, basi na mwingine anayo fursa ya kujishindia fedha taslimu au pia gari kama mimi, alisema Mchite.

Wakati huo huo, kampuni ya Airtel leo imechezesha droo ya nane ya Tesa Kimilionea ambayo ni droo kubwa kwa mwezi wa pili. Kwenye droo hiyo wamepatikana washindi wawili wakubwa waliojishindia fedha taslimu Tzs 10,000,000 na mwingine gari mpya aina ya Toyota IST. Huku washindi wengine 100 wikijishindia Tzs 100,000 kila mmoja na washindi wawili Tzs 1,000,000 kwa kila mmoja.

Mshindi aliyejishindia gari ya IST ni Abdallah Said Kilumbaki ambaye ni mkazi wa Kilwa Masoko mkoani Lindi wakati aliyejishindia Tzs 10,000,000 fedha taslimu ni Stella Mwaseba mkazi wa Yombo Vituka vijijini Dar es Salaam kwenye droo kubwa ya mwezi.

Washindi wa fedha taslimu Tzs 1,000,000 ni Masoud Issah wa mkoani Mwanza na Gerald John Nteza wa wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
Promosheni ya Tesa Kimilionea ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi wa pili na itafikia kikomo mwishoni mwa mwezi wan ne. Promosheni hii ni kwa wateja pamoja na wakala wote wa Airtel na inalenga kuhamashisha malipo kwa kutumia njia ya mtandao.

Mkurugenzi wa huduma wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kati kati) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa promosheni ya Tesa Milionea Mchita Yusuf Mchita (kushoto) kadi ya usajili wa gari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa mshindi wa promosheni hiyo kwenye droo kubwa ya kubwa. Promosheni ya Tesa Kimilionea ambayo ni ya miezi mitatu inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel kujishindia zawadi za pesa taslimu Tzs100, 000, Tzs1, 000,000 au promosheni kubwa ya Tzs10, 000,000 kila mwisho wa mwezi pale wanapotumia huduma yeyote ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando.


Mkurugenzi wa huduma wa huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kati kati) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa promosheni ya Tesa Milionea Mchita Yusuf Mchita (kushoto) funguo za gari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa mshindi wa promosheni hiyo kwenye droo kubwa ya kubwa. Promosheni ya Tesa Kimilionea ambayo ni ya miezi mitatu inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel kujishindia zawadi za pesa taslimu Tzs100, 000, Tzs1, 000,000 au promosheni kubwa ya Tzs10, 000,000 kila mwisho wa mwezi pale wanapotumia huduma yeyote ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando.





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post