Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mjimwema mjini Makambako mkoani Njombe umeunda umoja wa akina Baba,lengo ikiwa ni kukutana na kujadiliana changamoto zao zikiwemo za ndoa na uchumi ili kutambua wajibu wao na nafasi zao katika familia.
Akina Baba hao wamesema umoja huo utaenda kuwa msaada kwao katika kutatua changamoto hizo,kwani kupitia semina mbalimbali ambazo watapewa zitawawezesha kusimama katika nafasi zao.
Mwenyekiti wa umoja huo bwana Seth Vegulla amewataka wanaume wote kujiunga na umoja ili kukaa kwa pamoja na kuzungumza changamoto zinazowakabili ili kuepukana na adha zinazoweza kuwakumba ikiwemo za kujichukulia sheria mkononi kutokana na wanayofanyiwa kwenye ndoa zao.
Askofu wa dayosisi ya kusini Dkt. George Fihavango amesema katika zoezi la kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo wanawake wajane,vijana na akina baba wamebaini uwepo wa changamoto kwa kila kundi jambo ambalo linasababisha migogoro katika familia na jamii kwa ujumla.
"Lakini pia hawa wanawake wasifikiri wapo salama wakimiriki uchumi na kudharau wale wanaoitwa vichwa (wanaume) hiyo haitaleta amani wala furaha"
Akina Baba hao wamemchagua Seth vegulla kuwa mwenyekiti na Atukuzwe ilomo kuwa katibu wa umoja huo ili kuhakisha malengo ambayo wamejiwekea yanatimia kwa wakati.
By Mpekuzi
Post a Comment