KIJANA WA KITANZANIA ABUNI MASHINE YA KUPUKUCHULIA MAHINDI |Shamteeblog.


Kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakipata changamoto ya Upotevu wa mazao wakati wa mavuno hali ambayo imekuwa ikiwapa hasara kubwa na kushindwa kufikia malengo yao

Katika kutatua changamoto hiyo kijana wa Kitanzania Alfred Chengula ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya IMARA TECH amebuni mashine ya kupukuchua maindi yenye uwezo wa kudhibiti tatizo hilo

Akizungumza hivi karibuni jijini Arusha na waandishi wa habari pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH)waliofanya ziara katika kiwanda hicho Jijini Arusha alisema mashine hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wakulima kupukuchua mazao ya aina mbalimbali yakiwemo mahindi

Alisema kuwa mashine hiyo ni mkombozi kwa wakulima kwani inauwezo wa kupukuchua magunia 25 ndani ya lisaa limoja na kwa siku nzima magunia 200

Aliongeza kuwa mbali na mashine hiyo pia wamebuni mashine nyingine ya kuchakata na kubaraza nafaka mbalimbali kwaajili ya chakula cha mifugo

"Uwezo ya mashine hii ya pili unaweza kusaga magunzi na kupata pumba kwaajili ya kulisha kuku,ng,ombe,mbuzi,nguruwe pamoja na mifugo mingine
"alisema Chengula

Pia mashine hiyo inauwezo wa kukatakata majani,mabua,majani ya migomba katika vipande vidogo vidogo kwaajili ya mifugo

Pamoja na mafaniko hayo makubwa mkurugenzi huyo alisema wanajivunia zaidi kuweza kubuni,kutengeneza na kuziuza mashine hizo ndani ya ya Nchi

Mbali na kubuni mashine hizo, kampuni yake inafanya utafiti wa kina kabla ya kutoa mashine ili kuweza kujua kama zinaubora na kutumia kwa matumizi mengine

"Tumeanza utafiti, mashine ya kwanza ni hii ya kukamua mafuta ya parachichi kwaajili ya kuwasaidia wazalishaji wa mafuta na hili tunashirikiana vizuri na Avomeru Group "alisema Chengula

Aidha aliongeza kuwa wanafanya utafiti wa mashine kwaajili ya kumenya karanga na kusaga na mashine hizi watatumia mfumo wa sola ili ziweze tumika zaidi vijijini ambapo hakuna umeme ili waweze kujiajiri na kuboresha maisha yao

Changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni hupatikanaji wa fedha kwaajili ya kuboresha miundombinu kwaajili ya kazi

"Tunashukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania na waandishi wa habari kuja kututembelea leo na kuona juhudi zetu tunazozifanya tunaamini hili watalifanyia kazi "alisema Chengula

Licha ya watafiti kufikia mafanikio hayo na faida zilizoanza kupatikana ,ili lengo liweze kutimia ushirikishaji wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari Tume ya Taifa ya sayansi na Technolojia COSTECH na pia taasisi za fedha zinahitajika 

Mkurugenzi wa kampuni ya ImaraTech ya jijini Arusha Alfred Chengula akionyesha waandishi wa habari  mashine ya kupukuchua mahindi

Mkurugenzi wa kampuni ya ImaraTech ya jijini Arusha Alfred Chengula akiongea na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania Dkt,Philibert Luhunga aliyevalia suti mara baada ya kutembea kiwanda hicho kwa lengo la kuona na kujifunza


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post