Mwenge wa Uhuru waugomea mradi wa Pikipiki wilayani Wanging’ombe |Shamteeblog.



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu.Sahili Nyanzabara Geraruma amekataa kukabidhi Pikipiki kwa kikundi cha vijana kilichopo kata ya Ilembula wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe kutokana na kubaini dosari ya kutokuwepo kwa bima ya vyombo hivyo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo kwa vijana Ndugu.Geraruma amesema Mwenge huo hauwezi kukabidhi vyombo hivyo kutokana na kutokuwa na bima itakayowawezesha kusaidia afya zao wanapopatwa na majanga.

“Mwenge wa Uhuru kwa uatambuzi huo wa kuto kuwa na bima za umiliki wa vyombo vya moto utakuwa haupo tayari kutoa hizo PikiPiki kwa vijana wetu,bima zitakavyopatikana utaratibu mwingine ataendelea nao mkuu wa wilaya”alisema Geraruma

Aidha amesema serikali inajengwa na vijana hivyo haipo tayari kuona kijana anaangamia kwa sababu zisizokuwa za msingi.

“Vijana ni rasilimali watu na haipo tayari kumuona kijana anaangamia pasipo sababu za msingi”alisema Geraruma.

Tangu mbio za Mwenge wa uhuru zilipozinduliwa mkoani Njombe hapo April 2 mwaka huu na kukimbizwa katika halmashauri tatu mpaka sasa hakuna mradi ulioweza kukataliwa mpaka ulipokataliwa mradi huo wa Pikipiki.

 

Mmoja wa wakimbiza Mwenge kitaifa akizungumza na kikundi cha vijana wajasiriamali wanaofanya shughuli za ujasiliamali kupitia kusafirisha abiria kwa kutumia Pikipiki.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu.Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza mara baada ya ukaguzi wa kikundi hicho kilichopo Ilembula wilayani Wanging’ombe



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post