Na Mwandishi Wetu -Aliyekuwa Abuja, Nigeria
Rais Samia Suluhu Hassan, amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo ya Africa Road Builders–Babacar Ndiaye Trophy kwa mwaka 2022.
Tuzo hiyo inatolewa kwa watu mashuhuri barani Afrika ambao wameonyesha dhamira yao ya kuendeleza sekta ya miundombinu ya usafiri katika bara hilo.
Kamati ya uteuzi wa tuzo hiyo imempongeza Rais Samia kwa ungozi wake na namna Serikali yake ilivyojipanga kuwezesha sekta ya miundombiu nchini Tanzania.
"Uongozi wake binafsi, uwekezaji mkubwa na kujitolea" katika kupanua barabara na mtandao wa reli nchini Tanzania. "Tunatuma pongezi zetu za dhati kwa Rais Samia Hassan na watu wa Tanzania," alisema Msemaji wa Taasisi ya ARB, George Orido.
Amesema kamati ilibaini dola milioni 290 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia ufufuaji wa usafiri wa barabara, reli na anga nchini Tanzania. Pia ilizingatia mkataba wa dola milioni 172.2 uliosainiwa na Kampuni ya China Corporation Limited kuipatia nchi mabehewa ya kisasa ya mizigo 1,430 ili kutekeleza mpango kabambe wa shirika la reli la Tanzania (TRC).
Kutokana na hali huyo pia kamati ilibaini kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi wa kihistoria wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje kuzunguka mji wa Dodoma, ambapo mradoi huo ulizinduliwa na Rais Samia February 11, mwaka na kuhudhuriwa na Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika, Dk. Akinwumi A. Adesina.
Hivi sasa Rais Samia ni rais pekee mwanamke barani Afrika, ambapo aliingia madarakani Machi 2021, baada ya kufariki kwa mtangulizi wake, Rais John Magufuli, ambapo wakati huo yeye alikuwa Makamu wa Rais.
Kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika, chini ya Rais wa Benki hiyo, Dk. Adesina ambapo tuzo ya Wajenzi wa Barabara Afrika Babacar Ndiaye Trophy limeandaliwa na Acturoutes, jukwaa la habari kuhusu miundombinu na barabara barani Afrika, na Shirika la Media for Infrastructure and Finance in Africa (MIFA), mtandao wa wanahabari wa Afrika waliobobea katika miundombinu ya barabara.
Kwa mwaka 2021 Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alishinda tuzo hiyo.
Tuzo hiyo lilianzishwa kwa heshima ya Babacar Ndiaye, ambaye alikuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka 1985 hadi 1995.
Haya hivyo tuzo hiyo kwa mwaka 2022 litatolewa katika mkutano wa mwisho wa Wajenzi wa Barabara Afrika, ambao umepangwa kufanyika pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mei mwaka huu jijini Accra, nchini Ghana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto, wakiondoa kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma, Februari mwaka huu
By Mpekuzi
Post a Comment