RAIS SAMIA ATAKA SHULE YA UONGOZI MWALIMU NYERERE KUHIFADHI HISTORIA YA UHURU KUSINI MWA AFRIKA |Shamteeblog.


Khadija Kalili, Kibaha

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema ametoa Rai kwa Uongozi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kuwa kitovu Cha Kuhifadhia historia za nchi zilizopigania uhuru Kusini mwa nchi za Afrika.

"Andikeni historia ya nchi zilizopigania uhuru Kusini mwa nchi zilizopo Kusini mwa Afrika kwenye vitabu na pia muhifadhi ndani kwenye maktaba za Chuo ili Kizazi kijacho kiweze kusoma historia ilivyoandikwa na waasisi wetu" alisema Rais Samia.


Rais Samia amesema hayo leo ikiwa ni katika mdahalo wa maadhimisho miaka 100 ya kuzaliwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

"Siiku ya leo ni ya kipekee na historia katika nchi zilizopo Kusini mwa Afrika kwa kufanya kumbukizi ya kuzaliwa kwa aliyekuwa baba wa Taifa hiyo Hayati Julius Nyerere" alisema Rais Samia.

"Kumbukizi hizi zinafanyika katika sehemu sahihi kabisa ambapo tupo ndani ya Shule Kuu ya Siasa ya Mwalimu Nyerere kwani yeye alishirikiana na Hayati Abeid Amani Karume kuijenga nchi yetu na sote tumelikuta taifa letu na sisi tunaliendeleza binafsi nawiwa vigumu kueleza mambo yake mengi mema aliyoyafanya Mwalimu kwa sababu mada zote zilizowakilishwa na wanazuoni na watu waluowagi kufanya nae kazi wameelezea vya kutosha hivyo mimi sitaweza kuzungumza mambo makubwa na mema yote aliyoyatenda baba yetu kwani yote yaliyoelezwa yamemalizwa "alisema Rais Samia.

Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyoopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani Rais Samia amewataka watanzania kuyaishi mema yote aliyoyatenda Hayati Nyerere kwa nchi hii na bara la Afrika kwa ujumla.

"Binafsi somo kubwa alilotufundisha hayati Nyerere ni uzalendo ambapo alijitoa, aliacha kazi yake ya ualimu na kujikita katika harakati za kulikomboa taifa hili alipinga vikali udini, itikadi za siasa, udini"

"Tunakazi ya kurudi na kuifanya Tanzania kuwa moja huko nyuma tulitetereka na kujuana kwa itikadi, kikanda na kidini lakini sasa hatujachelewa turejelee katika imani yake ikiwemo kutumia lugha ya Kiswahili kuwa ya Kitaifa na mataifa"alisema Rais Samia.

"Aliamini kuwa Afrika ni moja na alikua mpiganaji aliyekuwa katika mstari wa kwanza katika kupigania ukombozi katika nchi zilizopo Kusini Mwa Afrika"alisema Rais Samia

Alisema kuwa anamshukuru mama Maria Nyerere na familia kwa ujumla sambamba na hilo amesema anapenda Chuo hili kiwe kitovu Cha Uandishi na historia za uhifadhi wa harakati ukombozi katika nchi zilizopo Kusini mwa Afrika.

Katika mdahalo huo wanazuoni waliochangia mada ni Professa Issa Shivji, watu waliowahi kufanya nae kazi baadhi Yao ni Balozi Mstaafu Getrude Mongela, Kanali Mstaafu Simba Kalia, aliyekuwa Waziri katika nyakati tofauti pia Mbunge wa wa Jimbo la Bunda Stephen Wassira.

Huku wengine waliohudhuria katika mdahalo huo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge huku Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akiwa ni mwakilishi wa familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambapo alipokea tuzo Heshima na kutambua mchango wa Nyerere.

Akizungumza wakati akimkaribisha Mheshimiwa Rais Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa shukurani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki katika mdahalo wa kuenzi miaka 100 yaliyohaa Utumishi wa kutukuka na kuwa miongoni mwa wanajumuia ya Afrika kuwa anatambulika na kuwa hatosahaulika

Pia ameutaka umma kuenzi na kurithisha falsafa zake ikiwamo kupiga vita ujinga,umasikini na maradhi.

Pia amewashukuru wanazuoni wote waliohudhuria mdahalo huu
pamoja na Mabalozi na Viongozi wa vyama 13 vya Siasa wanafunzi wa chuoni hapo pamoja na wananchi.


 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post