Katika kuboresha zaidi sekta ya afya hapa mchumi, Wizara ya Afya imepata kibali cha kuajiri Wataalamu 1650 wa vitengo mbalimbali vya Afya ambao wataajiriwa na kupangiwa kazi katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dr. Abel Makubi.
Profesa Makubi amesema kuwa utekelezaji huo ni ahadi iliyotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Vitengo vitakavyonufaika na nafasi hizi ni pamoja na Madaktari Bingwa (25), Madaktari (215), Wafamasia(15), Maafisa Maabara(62), Wateknolojia (Dawa, Maabara, Mionzi, Macho-155), Maafisa Uuguzi (140).
Vitengo vingine ni Maafisa Uuguzi Wasaidizi (467), Wauguzi (140), Wakemia (2), Madaktari wa Afya Kinywa na Meno (15), Tabibu Meno (19), Watoa Tiba kwa Vitendo (15), Wazoeza Viungo kwa Vitendo(31), Maafisa Wazoeza Viungo (33), Maafisa Afya Mazingira(40), Wasaidizi wa Afya (134), Wahandisi Vifaa Tiba (17), Wateknolojia Vifaa Tiba (40) na Watunza Kumbukumbu wa Afya (10) na Madereva (4).
The post Serikali kuajiri wataalamu wa afya 1650 first appeared on KITENGE BLOG.
The post Serikali kuajiri wataalamu wa afya 1650 appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment