Simba SC yafanya mauaji Dar, yatinga Robo Fainali CAF |Shamteeblog.




Klabu ya Simba SC ya Tanzania na RS Berkane ya Morocco zimetinga kibabe hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi katika michezo ya mwisho ya Kundi D.

Simba SC ikicheza uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam imeichapa US Gendarmerie ya Niger mabao 4-0 bao la kwanza likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 63.

Mabao mawili yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 huku bao la nne akijifunga mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu baada ya kushindwa kuutuliza mpira kurudishiwa na beki wake.

Berkane nao wameifunga ASEC Mimosas bao 1-0 likipatikana dakika ya 28 likifungwa na Chadrack Lukombe kwa Mkwaju wa Penati


 
Kwa ushindi huo Timu hizo zimemaliza zikiwa na alama 10 kila mmoja huku RS Berkane wakiongoza wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa nafasi ya tatu ikishikwa na ASEC Mimosas yenye alama 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa alama zao 5.


from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post